Mbunge Tanga Awaokoa Askari wa Jiji la Tanga kwa Kipigo…!

  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku. Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji …

Rais Kikwete Aaanza Kuaga Watanzania Tanga

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amewashukuru wananchi wa Tanga kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake hali iliyomwezesha kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo. Rais Kikwete amesema hayo katika Uwanja wa Mkwakwani Mjini TANGA tarehe 3 Augusti, 2015 wakati akiwaaga rasmi wananchi wa Tanga. “Naungana nanyi kujipongeza kwa hatua …

NSSF Yaendesha Kambi za Kupima Afya Bure Mkoani Tanga

SHIRIKA la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), litaendesha kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Tanga. Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa elimu na kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza. Zoezi hili …

Mashindano ya ‘Zig Zag Rally 2015’ Kufanyika Tanga Mei 3

Na Mwandishi Wetu, Tanga MASHINDANO ya mbio za Magari ya “Zig Zag Tanga Rally 2015” yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mkoani Tanga Mei 3 mwaka huu mzunguko wa pili kwenye yale ya Kitaifa chini ya ufadhili wa Zig Zag. Mashindano hayo watashindanisha umbali wa km 135 na yatakuwa na awamu tano, yatakayoanzia katika hotel ya Tanga Beach Resort na kupitia maeneo …

Janga Lingine Polisi, Askari Wanyang’anywa Silaha 2

JESHI la Polisi limeendelea kukumbwa na majanga ya askari wake kuvamiwa na kunyang’anywa silaha nyakati za usiku wakiwa kazini. Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya tukio lililotokea mkoa wa Pwani kuvamiwa Kituo cha Polisi na majambazi kuua askari na kupora silaha, Safari hii imetokea mkoani Tanga juzi ambapo askari wawili waliokuwa doria kwa kutumia pikipiki waliporwa silaha mbili aina …