Rais Kikwete RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali yake inazikumbuka ahadi zote zilizotolewa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na imejiwekea utaratibu wa kuzitekeleza. Rais Kikwete ameyasema hayo Julai 25, 2011 katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara ambako ameanza ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa Rais wa Tanzania na kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuongoza nchi yetu. “Nashukuru kwa …
Rea kutumia bil 100 kupeleka umeme vijijini
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kwenye banda la wakala wa usambazaji wa umeme vijijini (REA) kwenye maonesho ya Nishati na Madini Mnazi Mmoja. Ismail Ngayonga na Salama Juma-Maelezo WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imepanga kutumia kiasi cha sh bilioni 100 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme katika mikoa 16 nchini. Hayo yamebainishwa leo (jana) na Mkurugenzi wa huduma za …
Stamico yatenga mil 140 kuwasaidia wachimbaji wadogo
Banda la STAMICO ndani ya maonesho ya Nishati na Madini Mnazi Mmoja. Na Ismail Ngayonga na Mpoki Ngoloke-Maelezo SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limepanga kutumia kiasi cha sh milioni 140 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Lwamgasa uliopo wilayani Geita Mkoani Shinyanga. Hayo yamebainishwa leo (jana) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa …
Picha za matukio Wiki ya Nishati na Madini Viwanja vya Mnazi Mmoja
Mtaalamu kutoka kitengo cha Mazingira katika Wizara ya Nishati na Madini Bw Silinge akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nishati na Madini Prof. Abdulkarim Mruma (kushoto) ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania. Bi Carlotta Richter kutoka Tanzania Renewable Energy Association (TAREA) akimwonyesha moduli ya umeme nuru Mgeni rasmi katika siku ya …
Kuiona Shelisheli na U23 taifa sh 5,000/-
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U23) itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Shelisheli kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha. Kiingilio cha chini katika mechi hizo kitakuwa sh. 3,000. Kwa jukwaa kuu kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati …
Mbunge amuita mkuu wa mkoa mnyonyaji wa wakulima
Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara. Dodoma, MBUNGE Seleman Bungara wa Jimbo la Kilwa Kusini (CUF), amediriki kumuita Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Meck Sadiq kuwa ni mnyonyaji mkubwa wa wakulima wa zao la ufuta jimboni kwake. Mbunge huyo, amesema Sadiq na kundi lake la watu wachache wamekuwa wakiwalazimisha wauze ufuta wao kwenye Chama cha Ushirika Ilulu, ambacho kinanunua kwa …