MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA MKOANI MTWARA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108 waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za …

Arusha kwachafuka tena, FFU wapiga mabomu, virungu

Baadhi ya waandamanaji wakiimba na kucheza kabla ya kuzuka kwa vurugu na FFU kulazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi. Mwandishi Wetu, Arusha MADEREVA wa daladala (maarufu kama vifodi) mkoani Arusha jana walifanya mgomo wakupinga kitendo cha kutozwa fedha kiasi cha Sh 5,000 hadi 10,000 na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani hata kama magari yao hayana makosa. Walidai endapo baadhi …

MECHI YA SIMBA NA YANGA NGAO YA JAMII YASOGEZWA MBELE

MECHI ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012 kati ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Agosti 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa itafanyika Agosti 17 mwaka huu kwenye uwanja huo huo. Uamuzi huo umetokana na timu ya Taifa (Taifa Stars) kuwa na mechi ya kirafiki katika kalenda ya FIFA …

Picha mbalimbali za shughuli za kuagwa kwa marehemu Danny Mwakiteleko jijini Dar es Salaam

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Danny Mwakiteleko, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa msafara wa mazishi kuelekea Mbeya. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakiwa wamejipanga kabla ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Mwakiteleko nyumbani kwake Tabata Chang’ombe. Baadhi ya wambolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu, Mwakiteleko. …

Mamia wamuaga Danny Mwakiteleko Dar es Salaam

‘Pokea saluti mpiganaji, Danny Mwakiteleko’ baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwakiteleko. Na Mwandishi Wetu MWILI wa Marehemu, Danny Mwakiteleko umeagwa leo nyumbani kwake Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam na mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi. Baada ya taratibu za kutoa salamu za mwisho …

UVCCM wawalaani wanaojilimbikizia madaraka CCM

Benno Malisa Na Mwandishi Wetu, Dodoma BARAZA Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), limelaani kitendo cha wajumbe wa Halmashauri Kuu NEC ya CCM kujilimbikizia madaraka. UVCCM imependekeza wajumbe wa NEC, wasiwe na madaraka zaidi ya moja kwenye maamuzi ngazi ya kitaifa. Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa alitoa tamko hilo mjini hapa jana, katika …