Kupata ratiba kamamili ya Taifa Ngazi ya Taifa Fainali – 2011, tafadhali bofya hapa; Ratiba ya Taifa Ngazi ya Taifa Fainali – 2011 xx
RHINO SPORTS YAUZWA MBEYA
Halmashauri ya Jiji la Mbeya (Mbeya City Council) imeinunua timu ya daraja la kwanza ya Rhino Sports Club ya Arusha. Hivyo timu hiyo sasa makao makuu yake yatakuwa Mbeya na itaitwa Mbeya City Council Sports Club- MCC. Pia uongozi wa Halmashauri hiyo umemteua Kocha Juma Mwambusi kuwa Meneja wa timu hiyo na amepewa idhini ya kushughulikia usajili na taratibu nyingine …
MTIHANI WA UWAKALA WA FIFA IJUMAA
Logo ya FIFA MTIHANI wa Uwakala wa Wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 29 mwaka huu. Mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili; maswali kutoka FIFA na kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika saa 4 asubuhi. Kwa Watanzania wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wafike TFF ili waweze kupewa taratibu za mtihani huo …
Veta shirikianeni na wawekezaji-Kikwete
Rais Jakaya Kikwete Na Mwandishi Maalum, Mtwara RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameutaka uongozi wa Chuo cha Ufundi Stadi Kanda ya Kusini (VETA) kuwa tayari kupokea walimu na vifaa ya kisasa vinavyoletwa na wawekezaji kwa ajili ya sekta ya gesi na mafuta. Rais ametoa kauli hiyo jana mkoani Mtwara alipotembelea chuo hicho kwa ajili ya kuwaeleza nafasi iliyopo na makubaliano yaliyofikiwa …
Mwanamuziki maarufu Senegal akamatwa, raia wapinga
MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa kufokafoka (Hip Hop) nchini Senegal Omar Toure, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Rais Abdoulaye Wade, amekamatwa. Mwandishi wa BBC Thomas Fessy mjini, Dakar, anasema washabiki wake kadhaa wameandamana wakitaka aachiliwe huru. Polisi hawakutoa sababu za kukamatwa kwa Bw Toure, ambaye ni maarufu kwa jina la Thiat. Alizungumza katika mkutano wa hadhara wa wapinzani siku ya …
Matukio Ya Bungeni Dodoma Leo
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dkt. Anthony Mbassa (hayupo pichani) kuhusu Serikali kugawa maeneo mapya katika wilaya hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu Bungeni leo mjini Dodoma. Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda kulia akimsikiliza waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. …