Na Janeth Mushi, Arusha HATIMAYE mgomo wa daladala uliodumu kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Arusha umeisha jana na huduma hiyo ya usafiri kuanza kutolewa kama kawaida,ambapo awali jeshi la polisi mkoani hapa lililazimika kutumia mabomu ya machozi kwatawanya wapiga debe na madereva waliokuwa wakifanya fujo zilizosababisha uharibifu wa mali yakiwemo magari ya serikali na ya watu binafsi. Akizungumza …
Breaking News: Mbunge wa Chadema atolewa bungeni
Mbunge Wenje Dodoma, HABARI zilizotufikia muda huu kutoka bungeni mjini Dodoma ni kwamba; Mbunge wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika kikao kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Wenje ametolewa nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa …
Picha mbalimbali za mazishi ya Danny Mwakiteleko Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Rungwa Jackson Msome alikuwa mmoja wa viongozi waadamizi wa Serikali waliohudhuria ibada ya mazishi. Pichani Mkuu wa Wilaya hiyo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Danny Mwakiteleko. Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Deodatus Balile akiaga mwili wa mfanyakazi mwenzake ambaye alikuwa ni Naibu wake kazini, marehemu Mwakiteleko. Mke wa marehemu Mwakiteleko, …
Jalada la Chenge utata mtupu
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge HATIMA ya jalada la uchunguzi dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, bado ni kizungumkuti, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elieza Feleshi, kusisitiza jana kuwa mpaka sasa halijafika ofisini kwake. Lakini alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, alisema: “Kama hajalipata, atalipata …
Umeme waligawa baraza la mawaziri
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda *WANYOSHEANA VIDOLE KUMTAFUTA MCHAWI KAULI tofauti zinazotolewa na viongozi wa Serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya mawaziri kuhusu suala la mgawo wa umeme, zinaonyesha kutokuwapo uwajibikaji wa pamoja katika Baraza la Mawaziri.Uchambuzi uliofanywa na gazeti hili kuhusu sakata la tatizo sugu la mgawo wa umeme nchini unebaini kwamba, kauli za viongozi hao wa Serikali …
Maadui wa Serikali si Chadema, niwatendaji-Lusinde
Livingstone Lusinde Dodoma MBUNGE wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), amewalipua watendaji wa umma kwa kueleza kuwa ndiyo maadui wakubwa wa Serikali na siyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Amesema mipango yao isiyotekelezeka ndiyo inasababisha wananchi wakose imani na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lusinde alitoa kauli hiyo bungeni, wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato …