KLABU ya Majimaji ya Songea imeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikiondoa pingamizi ililoweka awali dhidi ya mchezaji Ulimboka Mwakingwe ambaye Simba imemuombea usajili kwa msimu wa 2011/2012. Majimaji kupitia Katibu Mkuu wake Henry Kabera imesema baada ya kukutana na uongozi wa Simba imeamua kuondoa pingamizi dhidi ya mchezaji huyo ambaye ilimsajili kwenye dirisha dogo msimu uliopita. Awali …
WENJE ATOLEWA KWA NGUVU, MBUNGE CCM ANUSRIKA KUPIGWA
Dodoma MBUNGE wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, jana alijikuta akitolewa bungeni na askari (wapambe) wa Bunge waliotii amri ya Mwenyeviti wa Bunge, Sylivester Mabumba, aliyeongoza kikao siku hiyo. Katika tukio ambalo ni la kwanza kutokea tangu kuanza kwa Bunge la Kumi linaloongozwa na Spika Anne Makinda, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alinusurika kupigwa na wabunge wa kambi ya upinzani …
Dk. Bilal aongoza mamia kumzika Prof. Samuel Mushi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Julai 27, 2011. Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, …
Meneja Mkuu UDA amlipua Massaburi
Didas Massaburi Na Mwandishi Wetu SIKU moja baada ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Massaburi kutoa madai ya kusimamishwa kazi kwa Meneja Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Victor Milanzi, meneja huyo ameibuka na kujibu kuwa madai hayo hayana ukweli bali yanalenga kumchafua na kummaliza. Hali kadhalika Milanzi amedai kuwa Meya huyo pia …
Rais Kikwete amtumia Rage salaam za rambirambi
Ismail Aden Rage Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Simba ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, Mheshimiwa Ismail Aden Rage kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mzee Jimmy Daniel Ngonya kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya …