Fedha za pembejeo zawatokea ‘puani’ maofisa Chato

Chato, MAOFISA wanne kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Kagera wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutafuna fedha za pembejeo za kilimo zilizotakiwa kupewa wakulima. Kati ya waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo yumo Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Robert Matungwa pamoja na wakala wa usambazaji pembejeo. Watuhumiwa wote walisomewa mashtaka hayo jana mjini hapa na mwendesha mashtaka wa polisi wilayani hapa, …

Breaking News: Ajali mbaya Moshi, 11 wafa 22 wajeruhiwa

Moshi, Taarifa zilizotufikia muda huu ni kwamba; ajali mbaya imetokea mjini Moshi katika barabara ya Kibosho ambapo magari takribani manne yamehusika katika ajali hiyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio jumla ya watu 11 hadi sasa wamepoteza maisha na wengine 22 kujeruhiwa. Chanzo chetu cha habari kinasema ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na basi dogo aina ya Fuso, ambalo …

Kamati ya Wanafunzi Ustawi wa Jamii yazungumza na wanahabari Dodoma

JULAI 21, 2011, Taasisi ya Ustawi wa Jamii ilifunga masomo (kufunga Chuo) kutokana na mgogoro baina ya Menejimenti na Wahadhiri. Mgogoro huo ambao Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo, Mlwande Madihi alisema umesababisha mgomo usio halali wa wahadhiri, umekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kukosa malazi na kushindwa kujikimu kimaisha huku wengine muda wao wa ruhusa kazini …

SARA DUMBA ASIFU JUKWAA LA ALIZETI

SARA DUMBA Na William Macha-Iringa MKUU wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba amelimwagia sifa Jukwaa la Alizeti lililozinduliwa mkoani Iringa, kupitia mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) lilowakutanisha wadau anuai wa masuala ya kilimo na tafiti. Akizungumzia jukwaa hilo, Dumba amesema wakulima wa alizeti mkoani Iringa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakizalisha mazao kwa uzoefu, lakini sasa wanapaswa kutumia nyenzo za …

KIKWETE AAHIDI KUMALIZA KERO YA MAJI NEWALA

RAIS Jakaya Kikwete amesema atalisimamia suala la maji koani Mtwara hadi kuhakikisha shida ya maji inakoma mkoani humo. Rais Kikwete amesema hayo wilayani Newala ambapo yuko kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua na kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuongoza tena Tanzania na pia kufuatilia utekelezaji wa ahadi alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita. “Kilio kikubwa mkoani hapa …

SHELISHELI, U23 WAINGIZA MIL 5/-

MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 na timu ya Taifa ya Shelisheli iliyochezwa jana Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha imeingiza sh. 5,014,000. U23 ilishinda mechi hiyo mabao 3-1. Timu hizo zitarudiana tena kesho (Julai 29 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo. Shelisheli iko …