Wanafunzi Wasomea Chini Waiomba Serikali Kuboresha Mazingira

ELIMU

Na: Woinde Shizza, Simanjiro

Mpango mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani jamii ya kifugaji kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.

Wanafunzi wa shule hii ya msingi Kichagare wamekuwa wanajisomea wakiwa wamekaa chini huku shule hiyo ikiwa imeezekwa na vipande vya turubai ili kuweza kupata ahueni wakati wakujisomea ambapolengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya teknolojia.

Mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Lilian Nanyaro ambapo alisema kuwa aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .

Alisema kuwa mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia kwamba watoto ambao ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.

‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani inafikia mahali wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana hivo wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema Nanyaro.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Seigulu James alisema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana ,kwani kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.

Alitumia fursa hiyo kuiomba serekali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi wengine na watoto wa shule zingine.

Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro alisema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo alisema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.

“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake alisema kuwa mapaka sasa tayari vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.

Wahenga wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.