Rais wa Marekani Trump Akiwa Ziarani Nchini Israel

    RAIS wa Marekani Donald Trump amewasili nchini Israel akiendelea na ziara yake ya kikazi katika maeneo ya Mashariki ya Kati ambapo pia anatarajiwa kuzuru Maeneo ya Wapalestina. Amefika huko akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, ambako alitoa hotuba katika mkutano mkuu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu. Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na …

Rais Barack Obama Atupia ‘Madongo’ Donald Trump

RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo ‘si marekani wanayohitaji.’ “Kuwabagua Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama, na kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu,” Obama alisema. Siku ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea …

Mitt Romney Amwita Mgombea Trump ‘Tapeli’

ALIYEKUWA mgombea wa urais kupitia Chama cha Republican nchini Marekani, Mitt Romney ameibuka na kukitaka chama chake kutomteuwa Donald Trump huku akimtaja mgombea huyo aliyeshinda kuwa ni tapeli. Romney ametoa shutuma hizo kwa Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari. Trump hatahivyo amemkejeli Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea …

Wanajeshi Wanne wa Marekani Wauwawa, 40 Walipuliwa Nigeria

MTU mwenye silaha amewaua askari wanne wa Jeshi la Majini la Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika Mji wa Chattanooga, Tennessee. Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maofisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo. Kufuatia …

Mapokezi ya Rais Kikwete Alipowasili Kutoka Marekani

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu Novemba 29, 2014.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu Novemba 29, 2014.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia …

Rais Kikwete Kurejea Nyumbani Novemba 29

ENDAPO ratiba ya madaktari wanaomtibu Rais Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani itakwenda kama ilivyopangwa kiongozi huyo atarejea nchini Tanzania, Novemba 29, 2014. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Taratibu za matibabu ya Rais Kikwete, zimekamilika Novemba 24, 2014. Taarifa hiyo imesema Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana …