WATU 10 wanahofiwa kupoteza maisha huku 34 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hood namba T.762 AVL aina ya Scania kuteketea kwa moto. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Joseph Lugila alisema ajali hiyo ilitokea katika Mbuga ya Mikumi baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso la lori lilobeba mafuta ya kupikia lililokuwa likitoka Morogoro kuelekea Iringa …
Azam FC kukipiga na Coast Union Tanga
Nembo ya Azam FC Na Jaffer Idd TIMU ya Azam FC Ijumaa inatarajia kwenda Tanga kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara Coast Union, mchezo unaotarajiwa kupigwa Ijumamosi katika uwanja wa Mkwakwani. Azam inakwenda Tanga kwa mwaliko maalum wa timu ya Coast Union, ambayo inajiandaa kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada …
Miss utalii Tanzania 2011/12 kuzinduliwa Dodoma
Mhifadhi katika Hifadhi ya Tarangire, Beatrice Kessy (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki Miss Utalii Tanzania 2011, katika ziara yao. BAADA ya kukamilisha uundaji mfumo mpya wa uongozi na uteuzi wa wakurugenzi 60 wa kamati ya Taifa hadi Wilaya wa Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha …
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ziara Rasmi ya kitaifa Afrika ya Kusini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Ulinzi la Afrika ya Kusini wakati wa mwanzo wa Ziara yake Rasmi ya kitaifa nchini Afrika ya Kusini .Mawaziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na Tanzania Bernard Membe na Bi. Maite Nkoana Mashabane wakibalishana mikataba ya kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano(Bi-National …
Chadema yasema vyama vyote vinafanya siasa vyuoni
Dodoma, MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), amesema siasa vyuoni hazitakoma, endapo Serikali itashindwa kuwatimizia wanafunzi haki zao. Alisema kila chama kinafanya siasa vyuoni na siyo kukitupia lawama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo pekee, kwamba kinafanya siasa vyuoni. Mbilinyi alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ya …
Wabunge wa CCM walivyovutana kabla ya kuiondoa bajeti ya Ngeleja bungeni, wapendekeza bosi Tanesco aadhibiwe
Baadhi ya wabunge wa CCM wakiwa bungeni Dodoma. Dodoma VUGUVUGU la kuondolewa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, lilianzia ndani ya kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo walivutana vikali kabla ya kuazimia kuitoa bungeni bajeti hiyo. Vyanzo vya habari kutoka katika mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma siku moja kabla ya Serikali kuiondoa bungeni bajeti hiyo; …