Wizara ya Nishati na Madini inaliaibisha Taifa-Wanaharakati

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP MUUNGANO wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu, maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), umepokea kwa mshtuko, mshangao na masikitika tuhuma za Katibu Mkuu, Wizara ya Madini na Nishati, za kuandaa mpango wa kukusanya pesa idara na wakala walio chini ya wizara yake, kwa ajili ya ‘kuhonga’ wabunge ili wapitishe bajeti …

Serikali yangu haitaweka lami Serengeti- Kikwete

Rais Jakaya Kikwete Pretoria, Afrika Kusini RAIS wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema Serikali yake haikusudii kujenga barabara ya lami kukatisha mbuga maarufu duniani ya Serengeti iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Rais Kikwete amesema kuwa kama yupo kiongozi ambaye amethibitisha wakati wote wa uongozi wake kuwa mtetezi mkubwa wa mazingira na kulinda mbuga za wanyama basi ni yeye mwenyewe. “Serengeti …

Rais Kikwete ashawishi wawekezaji wa zabibu kuja Tanzania

Zao la zabibu Pretoria, Afrika Kusini RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete Julai 20, 2011, alitumia siku ya pili ya ziara yake ya kihistoria Afrika Kusini kwa kutembelea na kushawishi wawekezaji wa kilimo cha zabibu na utengenezaji divai kutoka nchi hiyo kuwekeza katika kilimo cha zao hilo mkoani Dodoma. Aidha, Rais Kikwete ametembelea Kisiwa cha Robben, kilichoko …

Pinda asema taarifa za Jairo kujiuzulu ni uzushi

David Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dodoma, TAARIFA zilizotolewa jana na gazeti moja la kila siku kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amejiuzuru si za kweli Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amethibitisha hilo. Waziri Pinda amesema, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, naye amesikia taarifa za, Jairo kujiuzulu kwenye vyombo vya habari na si …

Waziri Mkuu awataka wabunge kuchangamkia maabara

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema wakati Serikali inajipanga kutekeleza mpango wa kuimarisha masomo ya sayansi shuleni, meza ya maabara inayohamishika inaweza kutumika kupunguza tatizo la uhaba wa maabara katika shule za sekondari nchini. Alitoa kauli hiyo jana (Julai 20, 2011) mara baada kuzindua rasmi meza ya maabara inayohamishika (mobile science laboratory table with equipment) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. …

Maonyesho ya kimataifa ya Utamaduni wa Kiafrika 2011 yalivyofana huko Ujerumani!

Umati wa watu wa rangi zote ukifurahia vimbwanga vinavyoendelea jukwaani Binti wa Lucky Dube, Nkulee Dube akionyesha vitu vyake kwenye maonyesho hayo Waziri wa Utamaduni na Michezo wa Trinidad & Tobago, Mh. Winston Peters akionekana ni mwenye furaha pia. Mh. Winston Peters ndiye aliyefungua maonyesho hayo kwa mwaka huu wa 2011. Mpiga picha, Angèle Etoundi Essamba akionyesha tuzo yake aliyopokea …