Ofisa wa Sudan Kusini auwawa

KIONGOZI wa wapiganaji wa Sudan Kusini, ambaye alitia saini mkataba wa amani na Serikali, ameuwawa katika hali ya kutatanisha. Wanachama wa kikundi cha Gatluak Gai wamesema ofisa huyo aliingia katika mtego wa Serikali na kuuwawa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Sudan Kusini imesema aliuliwa na wafuasi wake. Kanali Gai ni kutoka kabila la Nuer ambalo limekuwa likizozana …

Watu 92 wauwawa mashambulio ya kigaidi Norway

Majeruhi wakitibiwa barabarani katika mji mkuu wa Norway, Oslo POLISI nchini Norway, imearifu kwamba watu wasiopungua 92 wameuawa kutokana na mashambulio mawili ya kigaidi. Kati ya hao, 84 waliuawa kwenye kambi ya vijana ya chama cha Social Demokratik iiyopo katika kisiwa cha Utoya karibu na mji Mkuu wa Norway, Oslo. Watu hao walipigwa risasi na mtu aliejifanya kuwa polisi. Mshambuliaji …

Loveness ndie Vodacom Miss Kanda ya Mashariki 2011

Vodacom Miss Eastern Zone 2011, Loveness Flavian (katikati) akipunga mkono akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Asha Saleh (kushoto) na Mariaclara Mathayo aliyeshika nafasi ya tatu, baada ya warembo hawa kutangazwa washindi wa shindano hilo. Loveness aliwashinda warembo wengine 10.Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni katika shindano la Vodacom Miss Kanda ya Mashariki, iliyofanyika mjini Morogoro …

Ikulu yamteua mrithi wa Jairo Nishati na Madini

KATIBU Mkuu Kiongozi, Phillemon L. Luhanjo amemteua Eliakim Chacha Maswi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Luhanjo amefanya mabadiliko hayo jana baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, David Jairo, kupewa likizo kwa muda, ili kupisha uchunguzi katika ofisi yake, ambapo inadaiwa wizara hiyo ilizichangisha fedha taasisi zake kwa lengo la kutumika kushawishi bajeti ya wizara ipitishwe …

WAZIRI WA AFYA NA HUDUMA YA WATU WA MAREKANI

Rais Jakaya Kikwete (Kushoto) akichukua nafasi muda mfupi kbla ya mazungumzo na wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), kwenye ukumbi wa karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu) Rais Jakaya Kikwete (Kulia) na Balozi wa marekani nchini, Alfonso E. Lenhadrt (Kuloa) wakishuhudia wakati mke wa rais, Mama Salma, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa waziri wa Afya na …

JK akutana na waziri wa afya wa Marekani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya na Huduma ya Watu wa Marekani Mheshimiwa Kathleen Sebelius. Rais Kikwete ameishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada wake mkubwa unaotoa kwa Tanzania katika sekta ya Afya. “Marekani inaongoza kwa msaada wake katika sekta ya Afya, tunashukuru sana na kuja kwako Tanzania kumetupa nafasi ingine ya kusema tunashukuru”. …