RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kesho, (Agosti Mosi, 2011) anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Wiki ya Sherehe za Nane Nane na Maonesho ya Kilimo mwaka huu kwenye Uwanja wa Maonesho ya Kilimo wa Nzuguni, Dodoma. Shughuli kuu za Rais katika ufunguzi huo itakuwa ni kufungua Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane kwa hotuba rasmi …
Mawaziri wameonesha uzalendo kwa wanafunzi Ustawi wa Jamii
Na Mwandishi Wetu, Dodoma “KWA kauli hiyo, Kamati Maalumu hii ya dharura inapenda kuutangazia umma kuwa, Serikali imeyapokea vizuri maombi ya Kamati na pia, inawapongeza Mawaziri na waheshimiwa wabunge kutokana na ushirikiano na ukarimu walioionesha Kamati hii.” Ndivyo inavyosema sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamati Maalumu ya Dharura iliyoteuliwa na Mkutano Mkuu wa Wanafunzi wa Taasisi …
Tanzania kupambana na Chad mchujo Kombe la Dunia
UPANGAJI makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil umefanywa Julai 30 mwaka huu, jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke. Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura imesema, Tanzania …
Dk Shein awataka wafanyabiashara kuacha dhuluma Ramadhani
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wafanyabiashara kujenga imani ya kufanya biashara bila dhulumu ya bei, vipimo wala ubovu wa bidhaa wanazoziuza hasa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Dk. Shein ameyasema hayo wakati akitoa risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa …
UFUNGUZI KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM DODOMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma, leo Julai 31, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama. Picha na Muhidin Sufiani-OMR Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume …
SERENGETI FIESTA LEADERS; NI NYOMI YA KUFA MTU
Umati wa watu na mashabiki wa SERENGETI FIESTA wakishangweka katika tamasha hilo ndani ya viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam jana. Wasanii kibao walitumbuiza katika tamasha hilo linaloendelea kupata umaarufu kila uchao. Msanii wa miondoko ya bongo fleva, Linex kutoka jijini Mwanza akiwaburudisha mashabiki lukuki waliojitokeza kuhudhuria tamasha la mwendelezo wa msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta lililofanyika jana …