Mkuu wa shule na makamu wake wapokezana kufundisha shule nzima

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchuchuma Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa, Bw. Joseph Thomas Lugome (58) akionesha darasa la saba ambalo limekuwa likisomewa pia na wanafunzi wa darasa la sita kwa kupokezana kutokana na shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 200 kuwa na walimu wawili pekee (Picha na Francis Godwin) Na Francis Godwin (TGNP), Ludewa SHULE ya Msingi …

Wanakijiji Tanangozi waneemeka na mradi wa MUVI

Mmoja wa wakulima wa nyanya Kijiji cha Tanangozi, Iringa. Na William Macha, Tanangozi, Iringa WAKULIMA wa nyanya kutoka Kijiji cha Tanangozi, Wilaya ya Iringa Vijini, wameusifu mradi wa nyanya uliofadhiliwa na Asasi ya Muungano wa Wajasiriamali Vijijini (MUVI), kuwa umeanza kuwaletea mafanikio dhidi yao. Kauli hiyo imetolewa jana kijijini hapa na mmoja wa wakulima wa zao hilo, Bw. Mtokambali Ngimba …

Wafanyabiashara wa vitunguu Mbulu wawalama kupanda kwa ushuru

Wafanyabiashara wa vitunguu saumu eneo la Kariakoo Na Mwandishi Wetu WAFANYABIASHARA wasambazaji wa vitunguu saumu jijini Dar es Salaam wameulalamikia utaratibu mpya wa tozo za ushuru kwa bidhaa hiyo, unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ambao umepandisha kodi kwa kiasi kikubwa tofauti ilivyokuwa awali. Malalamiko hayo yametolewa jana jijini Dar es Salaam kwenye soko la wafanyabiashara hao eneo la …

CCM sasa ‘yaingilia’ utendaji wa EWURA

Na Joachim Mushi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezipinga sababu zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), za kupandisha kodi ya mafuta ya taa kwa kisingizio cha kudhibiti vitendo vya uchakachuaji vilivyokuwa vimeshamiri. Madala CCM imeiagiza Serikali kuhakikisha inatafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa nchini, kwa kuwa ndiyo nishati inayotumiwa na wananchi …