Rais Kikwete apokea hati za mabalozi

RAIS Jakaya Kikwete leo Ikulu ya Dar es Salaam, amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Ujerumani Bwana Klaus-Dieter Brandes na kuagana na balozi wa Saudi Arabia anaemaliza muda wake hapa nchini Ali Abdulla Al Jarbou. Mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho Rais amefanya mazungumzo na balozi Brandes na kumwambia Tanzania inashukuru kwa misaada thabiti ya Ujerumani …

DK BILAL ATEMBELEA SHAMBA LA ZABIBU DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia ngoma ya asili kabira la Wagogo, wakati walipowasili Kijiji cha Chilangali (ii) Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma leo Agosti 02, 2011 kukagua mradi wa kilimo cha Zabibu (FUNE) katika shamba hilo lenye ukubwa wa Hekari 300. Picha na Muhidin Sufiani-OMR …

NGORONGORO HEROES YAALIKWA COSAFA

TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) imealikwa kushiriki michuano ya umri huo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwaka Afrika (COSAFA) itakayofanyika kuanzia Desemba 1-10 jijini Gaborone, Botswana. Wachezaji wanaotakiwa kushiriki michuano hiyo ni wale waliozaliwa baada ya Januari 1, 1992. Timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kufikia Agosti 17 mwaka …

VILLA KUANZIA LIGI UGENINI

TIMU ya mpira wa miguu ya Villa Squad ya Dar es Salaam iliyopanda daraja msimu huu Agosti 20 mwaka huu itaanza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012 kwa kucheza ugenini dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Mechi nyingine za raundi ya kwanza zitakuwa kati ya Coastal Union na Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga), …

Wananchi: Tafiti za utawala bora za APRM zifanyiwe kazi

Ofisa Habari wa APRM Tanzania, Hassan Abbas Na Mwandishi Wetu, Dodoma Wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wamesema katika kuboresha na kuinua utawala bora nchini ni vyema Serikali ikafanyiakazi tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi zake hasa tafiti za utawala bora zinazofanywa na APRM. Wananchi hao walitoa maoni hayo kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la …