Na Mwandishi wa Jeshi la Polis- Pemba BALOZI wa Polisi Jamii nchini, Bi. Rahma Al-Kharoosi ametoa sh. milioni 10 fedha ambazo zitatumika kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya katika kituo cha kuhifadhia vijana walioathiriwa na dawa hizo. Sambamba na hayo, Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amewataka wananchi kuendelea kuwafichua wale wote waliopo kwenye mtandao wa …
Kheri ya Mfungo wa Ramadhani wadau wote!
WAISLAM nchini Tanzania tarari wameungana na wenzao duniani kote kuanza mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani. Uongozi na wafanyakazi wa dev.kisakuzi.com unawatakia Ramadhani njema!
Sakata la samaki wenye ‘sumu’: Japan yatoa tamko
WAKATI Serikali ya Japan ikikanusha kuwa samaki waliosafirishwa kuja nchini hawana aina yoyote ya mionzi hatari kwa binadamu, Tanzania imesema wizara tatu zinatarajia kukutana hivi karibuni ili kutoa tamko rasmi kuhusu samaki hao.Jumla ya tani 125 za samaki hao wanadaiwa kuwa na mionzi ya nyuklia ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu. Ubalozi wa Japan nchini, jana ulitoa taarifa kwa …
Malecela ataka uamuzi mgumu dhidi ya Lowassa, Chenge
Dodoma MWANASIASA mkongwe, Samuel John Malecela, amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua maamuzi thabiti ya kumalizana na dhana ya kujivua gamba kwa ama kutekeleza au kutangaza kuachana na mpango wa kuwatimua makada wa chama hicho wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi. Malecela ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), alitoa wito huo juzi …
Serikali yashusha bei ya mafuta
Dodoma, MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeshusha bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kunzia leo. Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Chuo cha VETA mjini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu alisema bei ya petroli imeshuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 9.17. Dizeli …
Picha mbalimbali za maonesho ya Nane Nane mjini Dodoma
Ofisa Mfuko wa Hiari wa Kujiwekea akiba uzeeni (GEPF), Aziza Selemani akitoa ufafanuzi kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane jana mjini Dodoma. Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha Eva Varelian (kushoto) na Alice Kihiyo (kulia) wakimhudumia mteja jana mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya nane nane yanayoendelea. Ofisa Uhisiano wa Mfuko wa …