Huu nao ni ubunifu!

Dereva wa bajaji (kushoto) inayozunguka mitaani ikiuza maji jijini Dar es Salaam ikiwa imeegeshwa huku gurudumu la mbele likiwa juu ya jiwe maeneo ya Sinza Mugabe leo. Eti huu nao ni ubunifu wa dereva ili kuhakikisha maji hayabaki kwenye tanki la maji ya bajaji hiyo. (Picha na Joachim Mushi)

Makamu wa Rais Dk Bilal alipohudhuria hafla ya Kilimo Kwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakatiti wa wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Makamu wa …