Janeth Mushi, Arusha WIZARA ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na wafadhili toka nchini Japan imeahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli kwa ajili ya kulala wakulima wanaotoka katika wilaya mbalimbali katika Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya maonesho ya wakulima (Nanenane). Hayo yalisemwa juzi mjini hapa na Waziri wa Kilimo Chakula na …
Poulsen awaita 20 kuunda Stars
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ugenini inayochezwa kwenye tarehe zinazotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA dates. Mechi itachezwa Agosti 10 mwaka huu. Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa; Shabani Dihile (JKT Ruvu) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa …
Dar ni kero tupu, petroli, diseli yatoweka na kugeuka lulu
Na Joachim Mushi WAFANYABIASHARA wa usafirishaji na wamiliki wa vyombo vya moto jijini Dar es Salaam leo wameendelea kuhaha wakitafuta nishati za mafuta ya dizeli na petroli huku na kule bila mafanikio. Kero hii ilianza tangu jana baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati za Maji na Mafuta (EWURA) kutangaza kushusha bei bidhaa za mafuta ya dizeli, petroli …
Taswa waandaa bonaza la michezo miaka 50 ya uhuru
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimeandaa bonanza maalum la kuwapongeza wanamichezo mbalimbali waliopata kuiletea sifa nchi katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Bonanza hilo litafanyika jijini Dar es Salaam Novemba 5, 2011 mahali patakapotangazwa, ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 9, 2011. Kikao …
Wauzaji petroli, dizeli waiweka pabaya Serikali ya JK
Rais Kikwete. WAFANYABIASHARA wa nishati za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini, sasa wanaiweka pabaya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kile kuonekana kugomea uamuzi uliotolewa juzi wa kushusha bei za nishati hiyo. Uchunguzi uliofanywa a waandishi wa mtandao huu jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa, umebaini kuwa wafanyabiashara wengi wamegoma kuendelea kutoa huduma hiyo …