Pinda ahofia utendaji wa viongozi wa Serikali, ataka wapimwe

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema kuna haja ya kuweka utaratibu maalum wa kuwapima viongozi wa Serikali ili kuona kama wanatekeleza kwa vitendo kauli ya Kilimo Kwanza. Ametoa kauli hiyo jana Agosti 5, 2011 akizindua maonesho na mashindano maalum ya mifugo katika Viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma, ambako maonesho ya Nane Nane yanaendelea. “Kiongozi ni lazima aoneshe …

Dk. Bilal ana kwa ana na Hamad Rashid Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Hamad Rashid, wakati walipokutana nyumbani kwa Makamu mjini Dodoma hivi karibuni. Katikati ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

FAINALI LIGI YA TAIFA KESHO

LIGI ya Taifa hatua ya fainali inaanza Agosti 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ikishirikisha timu 12 zilizogawanywa katika makundi matatu ya timu nne. Timu ya kwanza kutoka kila kundi na washindwa bora wawili (best losers)- watafanya jumla ya timu tano zitakazopanda Daraja la Kwanza. Kundi A lina timu za Polisi Morani (Arusha), Mgambo Shooting (Tanga), Samaria …

KOZI YA MAKAMISHNA WA MPIRA WA MIGUU

KOZI ya makamishna wapya kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Taifa na Kombe la Taifa itafanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-8 mwaka huu. Kwa wanaotaka kuwa makamishna ni lazima washiriki katika kozi ambapo ada ni sh. 10,000. Washiriki wanatakiwa kuwa waamuzi wastaafu na viongozi (administrators) wa mpira …

COMMONWEALTH SCHOLARSHIP COMMISSION IN THE UNITED KINGDOM

COMMONWEALTH SCHOLARSHIP COMMISSION IN THE UNITED KINGDOM INVITES APPLICATIONS FOR SCHOLARSHIPS FROM STUDENTS FROM DEVELOPING COMMONWEALTH COUNTRIES Hello Friends, Please Follow the link below it might be an Opportunity to your Relatives, Daughter, Sons or any one close to you to achieve their dream carrier. For more information visit:- http://dewjiblog.com/?p=3259 Wishing you all the best of Lucky.

Azam FC ziarani Uganda, Rwanda

TIMU ya Azam FC inatarajia kuondoka Jumatatu mchana na ndege ya Shirika la Ndege la Uganda kuelekea nchini Uganda na baadae Rwanda kukamilisha ziara yake ya maandalizi ya Ligi Kuu (VPL) inayotarajia kuanza August 20 mwaka huu. Azam itaondoka baada ya kumaliza mchezo wa mechi ya kirafiki kati yake na timu ya Polisi Dodoma inayotarajia kufanyika Jumamosi ya Agosti 6, …