Na Mwandishi Wetu JUMLA ya kesi 42 za ukatili dhidi ya wanawake vijijini huko Kusini Unguja na kaskazini Pemba zimefikishwa katika vyombo vya sheria. Kesi hizo zinahusu wanaume waliooa na kuwatelekeza watoto na wake zao, mimba za utotoni, ubakaji na waume kupiga wake zao. Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Mwezeshaji wa Mradi wa Kuwawezesha Wanawake Zanzibar (WEZA) unaohusisha Shehia 60, …
Wakulima watakiwa kuzingatia ushauri wa wataalam
Na Janeth Mushi, Arusha WAFUGAJI na wakulima nchini wametakiwa kufufanya shughuli zao kwa kufuata ushauri wanaopatiwa na wataalamu ili kuongeza uzalishaji pamoja na ubora wa bidhaa wanazozalisha. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mtaalamu wa Pembejeo za Kilimo na Dawa za Mifugo, kutoka kampuni ya Keenfeeder’s wasambazaji wa dawa za mifugo na kilimo, Anzamen Muro alipokuwa akizungumza na wakulima katika …
Makamu wa Rais aitaka APRM ifike Zanzibar
Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Ali Seif Idi ameshauri Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) uhakikishe kuwa shughuli zake zinaelezwa na kueleweka kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi visiwani humo ili kuufanya mpango huo ueleweka vyema. Balozi Seif alitoa ushuri huo alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje …
Chadema wafanya uamuzi mgumu, watimua madiwani wake watano Arusha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma KIKAO cha Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana kwa dharura Jumamosi na Jumapili mjini Dodoma kimefanya uamuzi mgumu kwa kuamua kuwafukuza uanachama madiwani watano wa chama hicho mkoani Arusha ambao wamedaiwa kupinga amri ya kamati hiyo. Madiwani waliotimuliwa uanachama hivyo kupoteza moja kwa moja nafasi zao za udiwani mkoani Arusha ni pamoja na Estomih Mallah, John Bayo, …
Naibu Waziri wa Fedha alipotembelea Banda la Wizara hiyo Maonesho ya Nane Nane Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha Pereira Silima (kulia) alipata maelezo jana juu ya mpango wa hiari kutoka kwa Ofisa Masoko Mwandamizi, James Mlowe (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya wakulima ya Nane Nane ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima (kulia) akipata maelezo juu ya madeni ya ndani kutoka kwa Mhasibu aliyechini ya …
SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Na Janeth Mushi, Thehabari Arusha SERIKALI kwa kushirikiana na taasisi binafsi imetakiwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kilimo hicho, badala ya kutegemea kilimo cha msimu ambacho si cha uhakika sana. Wakulima wengi nchini wamekuwa wakilima kwa kutegemea hali ya hewa (mvua) hali inayosababisha wakati mwingine kiwango cha uzalishaji kupungua. Changamoto hiyo …