Tanzania imetangaza kuisaidia Somalia kwa kutoa msaada wa tani 300 za mahindi, ili kuwasaidia kupunguza makali ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili kiasi cha wananchi milioni 3.5 wa Jamhuri hiyo Tanzania pia imeahidi kutoa misaada mingine kwa nchi hiyo kwa kadri uwezo wa nchi unavyoruhusu katika kuisaidia Somalia kukabiliana na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiusalama ambayo yamekuwa …
Kikwete ampokea Rais wa Somalia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jana, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Ndege iliyomleta Rais wa Somalia, iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini …
SIDO IRINGA KUTOA MAFUNZO YA USINDIKAJI
Na William Macha, Iringa SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda nchini (SIDO) mkoni Iringa linatarajia kutoa mafunzo ya usindikaji bora bidhaa za chakula hivi karibuni. Akizungumza ofisini kwake meneja mkuu wa shirika hilo mkoani hapa, Gervase Kashebo amesema mafunzo hayo ya usindikaji wa mchuzi, nyanya mvinyo pamoja na bidhaa nyingine zitokanazo na matunda ya msimu yatawalenga wajasiriamali kutoka mkoani Iringa. Aidha ameongeza …
MUVI yaanza kutoa elimu kwa wakulima Njombe
Na William Macha, Njombe MRADI wa Muunganisho wa Wajasiriamali Vivijini (MUVI) kupitia kitengo chake cha habari umeingia Njombe na kufanikiwa kuzungumza na wajasiriamali wa zao la nyanya na alizeti kutoka mkoani humo. Katika hatua ya kwanza kitengo hicho cha habari kimefanya ziara kwenye vijiji vya Igongolwa, Lyamkena, Ikwete, Kiumba, Itipingi, Ibiki, Mahongole, Kifumbe, Uselule na Imalinyi. Wajasiriamali kutoka katika vijiji …
Naibu Waziri awataka maofisa kilimo ‘kuishi’ vijijini
Na Janeth Mushi, Arusha MAOFISA ugani na kilimo nchini wametakiwa kuhama maeneo ya mjini na kwenda vijijini ili kuwasaidia wakulima na wafugaji mbinu anuai za kilimo cha kisasa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika sekta hiyo muhimu hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji, Nane Nane juzi na Naibu Waziri wa Tawala …