Na Mwandishi Wetu, VIINGILIO katika mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu kuanzia saa 2.00 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni kama ifuatavyo vitaanzia sh. 5,000 na kuendelea. Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, …
RC Machibya afungua mafunzo ya wakufunzi wa Sensa
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali mstaafu Issa Machibya (katikati) akifungua mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio itakayofanyika kuanzia Septemba 4 mwaka huu nchini kote. Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa sehemu mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa watu watakaoshiriki kuendesha Sensa ya majaribio. Wengine ni – Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu , Dk. Albina Chuwa …
Dk. Bilal akabidhi zawadi kwa washindi mashindano ya Qur-an
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Mufti …
Dk Shein atembelea vituo vya ununuzi karafuu Pemba
Na Rajab Mkasaba, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameendelea na ziara yake kisiwani Pemba kwa kutembelea vituo vya ununuzi wa karafuu pamoja na kambi za karafuu na kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kulirejeshea hadhi yake zao la karafuu. Dk. Shein alikuwa akiwaeleza wananchi wakiwemo wamiliki wamiliki wa makambi …
Kesi ya Mubarak yaendelea nchini Misri
ALIYEKUWA Rais wa Misri, Hosni Mubarak anatarajiwa kufika mahakamani kwa awamu ya pili ya kusikilizwa kwa kesi ya kihistoria dhidi yake. Rais huyo aliyeng’olewa madarakani ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na maafisa wengine sita wa ngazi ya juu. Watu hao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi mwezi januari mwaka huu. Ingawa …
Rais Kikwete atuma rambirambi kwa balozi Nhigula
RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Balozi na Mwanasiasa George Nhigula ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Agosti 13, 2011 katika Hospitali ya Mikumi, Magomeni, Dar es Salaam kwa matatizo ya figo. Mzee George Maige Nhigula ambaye alizaliwa Aprili 3, mwaka 1929, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, ameaga dunia akiwa na umri wa …