Wafanyabiashara Mpanda wasota wakisubiri treni

Mpanda, BAADHI ya wafanyabiashara wa mazao walioweka kambi katika kituo cha Reli cha mjini Mpanda, wakisubiri kusafirisha mazao yao wameingiwa na hofu ya uwezekano wa kuharibika kwa mazao yao na kupata hasara ya mamilioni ya fedha. Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana mjini hapa, wafanyabiashara hao walisema iwapo uongozi wa Shirika la Reli hautachukua hatua za haraka kuwezesha kusafirishwa …

NHC kuondoa nyumba ndogo mijini na kujenga maghorofa

Dodoma, SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lina mpango wa kuondoa nyumba ndogo katika maeneo yenye thamani kubwa yaliyojengwa holela mijini na badala yake kujenga maghorofa kukidhi mahitaji ya makazi. Taarifa hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alipokuwa akimkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuzindua ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Medeli mjini Dodoma. …

Dk. Shein awataka wananchi kuwafichua wanaofanya magendo ya karafuu

Na Rajab Mkasaba, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi Pemba kushirikiana na serikali kupambana na wanaofanya magendo ya karafuu kwani hawana nia njema na serikali wala nchi. Amesema kuwa iwapo mwananchi atauza karafuu zake kwa njia ya magendo ajue kwamba kipato kitakachopatikana hakitomsaidia yeye binafsi wala serikali. Dk. Shein aliyasema …

Kikwete Kigeugeu

Na Saed Kubenea -Anauma na kupuliza -‘Auchuna’ kuhusu ufisadi RAIS Jakaya Kikwete sasa ana sura mbili. Akiwa serikalini anauma. Akiwa kwenye chama chake anapuliza. Wachunguzi wa masuala ya siasa nchini wanasema ameonyesha kuwa kigeugeu, hali ambayo inaweza kungharibu hadhi ndani na nje ya nchi. Hayo yamedhihirika katika taarifa ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyotolewa juzi Jumatatu …

Bunge laambiwa nchi ipo hatarini!

Zitto akumbushia vita ya Kagera Kilango: Serikali ichukue hatua Makamba: Itasababisha vurugu Mnyika: Kuna rushwa kubwa WAKATI kukiwa na taarifa za kuwapo mkono wa baadhi ya wanasiasa katika kuhujumu Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, tatizo la mafuta nchini limeelezwa kuwa linahatarisha usalama wa Taifa huku wabunge wakisema litazua vurugu na kwamba ni kana kwamba nchi iko vitani. Maoni hayo ya …

Washukiwa wa machafuko ya London kufikishwa mahakamani leo

Ni washukiwa wa kwanza kushtakiwa kwa vifo vilivyotokea wakati wa machafuko ya jijini London. Watu jumla ya watano walikufa kwenye machafuko yaliyoanza Jumamosi iliyopita. Mwanamume mmoja pamoja na kijana wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama moja ya Birminghman leo kuhusiana na mauaji ya wanaume watatu waliogongwa na gari wakati walipokuwa wakikilinda kitongoji chao dhidi ya waporaji. Ni washukiwa wa kwanza kufikishwa mbele …