RAIS wa Ufaransa Nicholas Sarkozy na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel wametoa mapendekezo mapya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaokabili mataifa yanayotumia sarafu ya Euro. Viongozi hao wanataka mfumo mpya kusimamia uchumi wa ulaya Baada ya kukutana mjini Paris, viongozi hao walitoa wito wa kile walichokitaja kuwa usimamizi mpya wa kiuchumi na kuyataka mataifa yanayotumia sarafu hiyo kusawazisha bajeti zao. …
Stars, kuikaribisha Algeria Mwanza
MECHI ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza. Bonifase Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema leo …
Uefa wamkalia kooni Wenger
ARSENE Wenger huenda akakabiliwa na hatua zaidi za nidhamu kutoka Uefa baada ya kuthibitishwa mawasiliano yake na benchi la ufundi la Arsenal yanachunguzwa. Wenger alikuwa akitumikia adhabu ya kutokaa kwenye benchi la timu hiyo wakati wa mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Udinese. Arsenal ilikuwa inahisi Wenger huenda angeruhusiwa kupitisha ujumbe kwa msaidizi wake Pat Rice kwa …
Misaada yazidi kumiminika Somalia
Jumuiya ya nchi za kiislamu imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 350 kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia. Ahadi ya msaada huo ilitolewa baada ya mkutano uliofanyika mjini Istanbul uturuki ambao ulihudhuriwa na Rais wa Somalia Sheikh Sharrif Sheikh Aden. Akizungumza kwenye mkutano huo waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema hatua ya kujitolea kusaidia …
Maelfu waandamana kupinga ufisadi India
Maelfu ya raia wa India wamejitokeza mitaani kumunga mkono mwanaharakati wa kupinga ufisadi Anna Hazare wakiwa na mabango yaliyoikemea na kuishinikiza Serikali imwachie huru. Mwanaharakati huyo,Bw Hazare anashinikiza kufanyika kwa mageuzi katika sheria za kupambana na rushwa na amepanga kuanza kukesha bila kula ili kushinikiza hilo lifanyike. Mwanaharakati huyo mwenye miaka 74, anapinga mswada uliowasilishwa bungeni kwa kuwa waziri mkuu …