Msimu mpya Ligi Kuu kuanza kesho, timu 10 kupambana

Na Mwandishi Wetu MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/12 unaanza kesho, Agosti 20 mwaka huu, ambapo timu 10 kati ya 14 zinazoshiriki katika ligi hiyo zitakuwa viwanjani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amezitaja mechi za kesho ni pamoja na Coastal Union Vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga), Kagera …

CHADEMA yazuiwa kufanya mikutano

Na Janeth Mushi, Arusha MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imetoa umauzi mdogo wa kuzuia kwa muda mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kile mikutano hiyo kuwazungumzia madiwani wake watano waliofukuzwa uanachama hivi karibuni. Mahakama imesema hata kama CHADEMA itapewa kibali cha kufanya mikutano basi kitakuwa na masharti ikiwemo kutolizungumzia suala la madiwani hao na kutotoa …

Kufanya Mapinduzi ya Kilimo ni dhamira ya SMZ- Dk. Shein

Na Rajab Mkasaba, Zanzibar MAPINDUZI ya kilimo ndio mwelekeo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba yenye nia ya kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kumkomboa mkulima wa Zanzibar kutoka kilimo duni na kumjengea fursa ya kupata tija na uhakika wa chakula. Uongozi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili iliyasema hayo katika kikao maalum na Rais wa Zanzibar …

Kashfa Maliasili na Utalii; Mkurugenzi asimamishwa kazi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI imemsimamisha kazi, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Obed Mbangwa na wasaidizi wake wawili kutokana na kashfa ya kusafirishwa wanyama hai nje ya nchi lililoikumba Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2010. Uamuzi huo ulitangazwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wakati akifanya majumuisho ya hotuba yake ya Makadirio ya Mapato …

Waziri Mkuu wa Uturuki ziarani Somalia

WAZIRI Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuwasili nchini Somalia kuanza rasmi kampeni ya kukabiliana na baa la njaa nchini humo. Waziri huyo katika ziara yake, ataandamana na Waziri wake wa Mashauri ya Nchi za Kigeni pamoja na wake zao. Viongozi hao wamesema wanakwenda nchini Somalia kuonesha wanawaunga mkono raia wa Somalia katika hali ngumu inayolikabili nchi hiyo. Hadi …