Tanzania yapiga marufuku uuzaji wanyamapori

Tanzania imetangaza kupiga marufuku biashara ya kukamata na kuwasafirisha wanyamapori kwenda nje ya nchi. Hatua hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja bungeni kuhusu madai kwamba wanyama takriban 130 wakiwemo ndege 16 walitoroshwa kinyume cha sheria mwishoni mwa mwaka jana na kusafirishwa kwenda nchi moja ya Mashariki ya Kati. Katika jibu lake Bw Pinda alisema: “Kwanza tunataka …

Longo longo za upatikanaji umeme nchini zaendelea

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU HALI YA UMEME NCHINI, WIKI HII Taarifa hii imewasilishwa jana bungeni Dodoma Mheshimiwa Spika, jana asubuhi, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika, Mheshimiwa Ezekiah Dibogo Wenje, Mbunge wa Nyamagana, alisimama kuomba Mwongozo wako, na akatoa taarifa kwamba kuna ukosefu mkubwa wa umeme katika Jiji la Mwanza kwa muda wa siku nne. Pia alieleza kuwa …

Dk. Bilal asaini makubaliano ya itifaki za SADC kudhibiti fedha chafu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maafikiano yaliyotokana na itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu udhibiti wa fedha chafu na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SADC yaliyoafikiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC mjini Luanda Angola Agosti …

Wakili Mwale apelekwa Gereza la Kisongo

Na Janeth Mushi, Arusha HATIMAYE wakili maarufu mkoani hapa, Medium Mwale anayeshtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi wa zaidi ya sh. bilioni 18 na kughushi nyaraka aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mt. Meru kwa matibabu amepelekwa mahabusu katika Gereza Kuu la Mkoa la Kisongo. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya …

Timu washiriki Ligi Kuu kulamba mil 26.3 kila moja

Na Mwandishi Wetu KILA timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajia kupewa jumla ya sh. milioni 26.3, fedha zitakazotumika kama gharama ya klabu katika mashindano hayo. Akizungumza na vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema fedha hizo zitatolewa kwa awamu tano tofauti kuanzia mwezi huu. Aidha Wambura alisema kwa Agosti kila timu …