Na Janeth Mushi, Arusha JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu saba wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, ambao walikutwa na bunduki mbili moja ikiwa ni SMG iliyokuwa na risasi 27 pamoja na bastola yenye risasi 4. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye alisema watuhumiwa hao wamekamatwa …
Fifa yaruhusu ITC ya Kago itolewe
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeruhusu Shirikisho la Mpira wa Miguu Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa mchezaji, Gervais Anold Kago aliyejiunga na timu ya Simba kutoka Olympic Real de Bangui ya huko. Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na TFF leo, FIFA imeruhusu ITC itolewe baada …
African Lyon kuwalipa Komba, Masenga kwa viingilio
Na Mwandishi Wetu TIMU ya African Lyon imeomba kuwalipa kwa makato ya mlangoni wachezaji wake wawili wanaoidai; Godfrey Komba na Abdul Masenga ambao ilikatiza mikataba yao msimu uliopita. Awali Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliiagiza Lyon kuwalipa wachezaji hao kufikia Agosti 17 mwaka huu vinginevyo isingeruhusiwa kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom iliyoanza leo, Agosti 20 mwaka huu. …
Majeshi ya NATO yakabidhi ulinzi kwa Afghanistan
Afghanistan imeanza utaratibu wa kuchukua madaraka ya usalama yenyewe, na jimbo la Banyan limekuwa la mwanzo kukabidhiwa na jeshi la NATO kwa polisi wa Afghanistan. Bamiyan, karibu na sanamu ya zamani ya Budha Mawaziri wa Afghanistan na mabalozi wa nchi za nje walihudhuria sherehe hiyo katika jimbo la kati. Mwandishi wa BBC nchini Afghanistan, anasema Bamiyan ni moja kati ya …
Vifo vya askari wa Marekani vyaongezeka Afghanistan
Askari wa Jeshi la Marekani wameendelea kuteketea na kufikia askari 31 ikilinganisha na mapema miezi iliyopita hii ni kutokana na kuanguka kwa helkopata ya jeshi lao kuanguka. Wakuu wa Afghanistan wanasema wanajeshi 31 wa Marekani na wanajeshi kadha wa Afghanistan walikufa, wakati helikopta yao ilipoanguka mashariki mwa nchi hiyo. Hiyo ni hasara kubwa kabisa kuifika Marekani katika tukio …
Afghanistan yashambulia ofisi ya Uingereza, Kabul
Washambuliaji waliojitoa mhanga wameshambulia afisi za British Council katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kuwaua takriban watu tisa na kushikilia eneo la Ofisi hizo kwa saa kadhaa. Bomu liliotegwa ndani ya gari liliangamiza ukuta unaozingira ua na watu kadhaa waliokua wamebeba silaha nzito wakavamia sehemu za ndani. Baada ya mapambano ya saa kadhaa Balozi wa Uingereza mjini Kabul alisema …