Mbunge apata ajali Dodoma, mkewe afariki dunia

Na Mwandishi wetu, Dodoma MBUNGE wa Baraza la Wawakilishi (B.L.W) wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mussa Khamis Silima amefiwa na mkewe baada ya gari alilokuwa akisafiri nalo kupata ajali likitokea Morogoro kuja mjini Dodoma. Akizungumzia tukio hilo jana bungeni Dodoma, Spika Anne Makinda aliliarifu Bunge kuwa ajali hiyo iliyosababisha kifo ilitokea juzi majira ya saa 1:45 usiku eneo la …

Msekwa ajibu mapigo, amuita mbunge wa CCM mzushi, anachuki

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MWENYEKITI wa Bodi ya Ngorongoro, Pius Msekwa amesema tuhuma zilizotolewa bungeni na Mbunge wa Ngorongoro, Kaika Telele wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa alikimbia mjadala bungeni na kwenda kugawa maeneo kwa wawekezaji ya ujenzi wa hoteli ni za uongo na uzushi. Msekwa amesema huenda mbunge huyo ameamua kumpakazia maneno hayo ya uzushi kwa chuku kwa kile, …

TFF yawashtaki Rage, Sendeu Kamati ya Nidhamu

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepeleka mashtaka mbele ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu. Taarifa hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na kuongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada …

Mlinzi aiibia Precision Air zaidi ya mil 35 Arusha

Na Janeth Mushi, Arusha MLINZI wa Kampuni ya Ulinzi ya Mint Master Security, aliyefahamika kwa jina moja la Hassan anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuiibia Kampuni ya Ndege ya Precision Air zaidi ya Sh. milioni 35.193 na Dola za Marekani 7,702 ambazo ni mauzo ya tiketi ya siku mbili ya shirika hilo. Akizungumza na waandishi …

Happy birthday Jerome Risasi

MDAU na Mwanafamilia wa tasnia ya habari Jerome Risasi leo anasherehekea siku ya kuzaliwa. Uongozi na wafanyakazi wa dev.kisakuzi.com unamtakia kila lililo jema, katika kuliendeleza gurudumu la kupashana habari nchini hasa kwa njia ya mtandao (new media). Ufuatao ni ujumbe alioutoa katika kusherehekea siku hiyo:- “Habari Mablogger, Mdau wenu ambaye naiendesha kwa karibu Blog ya www.theeastafrica.blogspot.com JEROME RISASI nasherehekea siku …

AJAAT, TACAIDS kuwashindanisha waandishi habari za Ukimwi

Na Esther Muze na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es Salaam CHAMA cha Waandishi wa Habari za UKIMWI (AJAAT) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) kimeanzisha shindano la miezi mitatu la uandishi wa makala za UKIMWI kwa mwaka 2011. Akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo mjini hapa, Mwenyekiti wa AJAAT, Simon Kivamwo amesema kuwa washiriki wa shindano …