Siku za Gaddafi za hesabika

Rais wa Marekani Barack Obama amesema utawala wa Gaddafi umefikia ukingoni na kumtaka aondoke madarakani ili kuepusha damu zaidi kumwagika. Amewataka waasi kuheshimu haki za binadamu, kuonyesha uongozi mzuri, kuhifadhi taasisi za Libya na kuelekea katika demokrasia. Mapigano makali yanaripotiwa kuendelea katika mji mkuu Tripoli, huku utawala wa Gaddafi ukiapa kuulinda mji huo dhidi ya waasi. Waasi nchini Libya wameingia …

Tripoli yachukuliwa na Waasi, mtoto wa Gaddafi akamatwa

PICHA za televisheni zinaonesha Waasi wakiwa katika Uwanja wa Green Square ndani ya Mji Mkuu, huku makundi ya watu wenye furaha wakisherehekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo. Taarifa zinaeleza Waasi wamemkamata mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam, huku kiongozi mwenyewe akiahidi kuwa ataendelea kupigana. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita, Luis Moreno Ocampo amethibitisha Saif al-Islam, mwanawe …

JK: Uongozi ni utumishi wa wananchi

Na Mwandishi Maalumu, Lindi RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kazi kubwa ya viongozi ni kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo na kero za wananchi, na si vinginevyo, kwani uongozi ni utumishi wa wananchi. Amesema kila kiongozi kwa ngazi yake ana wajibu wa kukabiliana na kumaliza matatizo na kero za wananchi walio chini yake, badala ya kusubiri uongozi wa juu …

NMB kutoa mikopo kwa wajasiriamali

Na Mwandishi Wetu, Iringa MUUNGANO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umefanikiwa kuwaunganisha wajasiriamali mkoani Iringa na Benki ya NMB mkoani humo, ili kuwasaidia kujipatia mafaniko zaidi katika kilimo. Akizungumza na wajasiriamali hao, Mratibu wa MUVI mkoa huo, Wilma Mwaikambo Mtui (pichani juu), amesema changamoto kubwa inayowakabili wakulima wengi ni upatikanaji wa mbegu pamoja na pembejeo za kilimo, hivyo kitendo cha kuwanganisha …

Dk. Bilal awazawadia washindi wa kuhifadhi Qur-an

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Jahuddi n Adam, kutoka Sudan, baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika Agosti 21 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed …

Yanga yachezea kichapo tena, Simba yatafuna tena

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam jana imeendelea kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kujikuta ikifungwa tena na Timu ya JKT Ruvu kwa bao moja kwa mtungi. Yanga ambayo jana mjini Morogoro ilionekana kucheza kwa kuzidia karibuni muda wote wa mchezo, ilijikuta ikifungwa goli moja kwa njia ya penati baada ya mmoja wa washambuliaji …