Diwani amkana DC mkutanoni

Na Mwandishi Wetu, Ludewa DIWANI wa Kata ya Ludewa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Monica Mchiro, amemkana hadharani Mkuu wa Wilaya hiyo, Georgina Bundala. Sakata hilo limetokea mjini Ludewa baada ya mkuu huyo kushindwa kuweka bayana kilichotokea kati ya wananchi na watafiti wa madini walioanza shughuli katika ardhi ya Kata ya Iwela bila taarifa …

Dk shein amzika Mbunge Silima

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza mazishi ya marehemu Mhe. Mussa Khamis Silima, Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Katika mazishi hayo yaliyofanyika kijini kwao marehemu huko Kiboje Mwembeshauri Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja viongozi mbali mbali walihudhuria akiwemo Makamu …

Viongozi Chadema kuburuzwa mahakamani Arusha

BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuwashikilia viongozi wawili wa CHADEMA akiwemo aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, Gervas Mgonja kwa wiki moja kwa tuhuma za kukutwa na silaha na kushiriki matukio kadhaa ya uhalifu wa kutumia silaha leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu madai yanayowakabili. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Ibrahim …

Jinamizi la muziki wa dansi lafunika Ulaya!

KUNDI la Ngoma Africa Band aka ‘FFU’ Ughaibuni, linatarajiwa kuendelea kumwaga burudani zake Ulaya na safari hii ni kwa mashabiki wa mjini Tuttlingen, show itakayofanyika Jumamosi ya Agosti 27, 2011 Bendi hiyo maarufu kwa muziki wa dansi barani Ulaya yenye maskani yake nchini Ujerumani, inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa la Afrika Festival, mjini Tuttlingen, Ujerumani ya Kusini, Kamanda Ras …

Uholanzi yaipiku Hispania ubora wa soka

Uholanzi imeipiku Hispania katika nafasi ya kwanza ya ubora Fifa wa kusakata soka duniani, huku Englan ikipanda nafasi mbili juu hadi ya nne. Wachezaji wa Uholanzi Hispania mabingwa wa soka duniani na Ulaya, wameporomoka hadi nafasi ya pili baada ya kupoteza pointi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia. England, licha ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Uholanzi kuahirishwa, …