Maofisa wa Polisi Burkina Faso wafungwa

MAOFISA polisi watatu wametiwa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika kwenye mauaji ya mwanafunzi kutoka Burkina Faso mwezi Februari, na kuchochea ghasia kwa wiki kadhaa. Justin Zongo alifariki dunia baada ya kudhalilishwa akiwa mikononi mwa polisi. Awali serikali ilisema kifo chake kilisababishwa na homa ya manjano, na kusababisha hasira miongoni mwa wengi. Maandamano- yaliyozidi kupamba moto kutokana na …

Sijiuzulu ng’o-Meya wa Jiji la Arusha

Na Janeth Mushi, Arusha MEYA wa Manispaa ya Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo amesema hawezi kujiuzulu wadhifa wake huo na kukanusha vikali kwamba hajavamiwa na majambazi kama taarifa zilivyovumishwa na baadhi ya watu wanaodai alitishiwa kuuwawa alipovamiwa nyumbani kwake. Ametoa kauli hiyo leo mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ukiwemo uvumi huo. …

Joice ataka kifo cha mumewe kichunguzwe

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joice Maimu ametoa wito wa kufanywa uchunguzi wa kifo cha mume wake Solomon kilichotokea wiki iliyopita kwenye shamba lao. Aliyekuwa mkuu wa majeshi, Jenerali Mujuru alikuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwenye chama cha Robert Mugabe cha Zanu-PF. Mwandishi wa BBC alisema kifo chake kimeibua wasiwasi kuwa huenda aliuliwa, na kusababisha mpasuko ndani ya chama …

Jairo apokelewa kama mfalme ofisini, gari lake lasukumwa, aimbiwa nyimbo

Na Joachim Mushi KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amepokelewa kama mfalme alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kurejea kazini baada ya kuchunguzwa na kuonekana hana kosa dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake kutokea bungeni. Jairo aliwasili katika ofisi za wizara hiyo majira ya saa tatu na dakika 16 asubuhi ya leo na kupokelewa …

CCM yasema malalamiko ya Rostam hayainyimi ‘usingizi’ Igunga

Na Joachim Mushi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema malalamiko aliyoyatoa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz pindi anajiuzulu hayawezi kuwanyima ushindi katika uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika ili kuziba nafasi hiyo baada yam bunge huyo kujiuzulu. Akizungumza na dev.kisakuzi.com leo katika mahojiano, Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema chama hicho kina utaratibu maalumu wa …

Nasri rasmi kukiputa Man City

Manchester City wamekubaliana na Arsenal kumsajili kiungo Samir Nasri. Nasri sasa anaelekea mjini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya. Nasri alifanya mazoezi na Arsenal siku ya Jumanne asubuhi kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Udinese, utakaochezwa Jumatano. Hata hivyo jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wachezaji. Kiungo huyo kutoka Ufaransa anakwenda Manchester pia kukamilisha mkataba wake …