JK amsimamisha tena Jairo, ni kupisha uchunguzi

Na Mwandishi Wetu RAIS Jakaya Kikwete amemsimamisha tena Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kupisha uchunguzi ambao utafanywa na Kamati Maalumu ya Bunge juu ya tuhuma zinasomkabili kiongozi huyo. Jairo amesimamishwa ikiwa ni siku moja tu baada ya kuanza kazi akitokea mapumzikoni alipokuwa amesimamishwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kupisha uchunguzi uliofanywa na Mdhibiti na …

Ofisa ugavi mahakamani kwa kugushi vyeti vya taaluma

Na Janeth Mushi, Arusha ALIYEKUWA Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Elizabeth Kisanga jana amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kwa kosa la kugushi vyeti vya sekondari na vya taaluma ya ugavi, kinyume cha taratibu na sheria. Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya hiyo, Devotha Msofe, Wakili wa Serikali, Sabina Silayo, aliieleza Mahakama kuwa …

Poulsen awaita 12 kuivaa Algeria

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen jana, Agosti 25 ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon. Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). …

Viongozi Chadema wafikishwa mahakamani kwa ujambazi

Na Janeth Mushi, Arusha KATIBU wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Wilaya ya Arusha, Anold Kamdye na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Gervas Mgonja, jana wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Agustine Kombe alidai kuwa …

Utumishi Zanzibar wamuunga mkono Dk Shein

Na Rajab Mkasaba, Zanzibar WIZARA ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeahidi kuunga mkono juhudi na bidii anazochukua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kufanikisha maendeleo ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira bora Watumishi wa Umma na kuimarisha Utawala Bora. Uongozi wa Wizara ya Nchi …

Wajasiriamali Tanga watakiwa kuungana

Na Mwandishi Wetu, Tanga WAJASIRIAMALI mkoani Tanga wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) ili kufanikisha lengo la kuunganisha nguvu za wajasiriamali na hatimae kujikwamua na umasikini. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Ndibalema Kisheru katika uzinduzi wa shughuli za wadau wa habari wa mradi wa MUVI mkoani hapa. …