WIZARA ya Ulinzi ya Uingereza imesema, ndege za kijeshi za Uingereza zimerusha mabomu kwenye handaki kubwa lililopo Sirte mji alipozaliwa Kanali Muammar Gaddafi. Ndege hizo ziliondoka kutoka kambi ya jeshi iliyopo Nolfolk siku ya Alhamis usiku. Waasi wa Libya nao wanaimarisha majeshi yao kwenye barabara inayoelekea Sirte, wakipeleka vifaru na makombora. Viongozi wa waasi wamezitaka serikali za kigeni kuondoa tanji …
Mama Salma ataka wanawake wajasiriamali wasaidiwe
Na Anna Nkinda – Maelezo WADAU wa maendeleo nchini wametakiwa kuwasaidia wanawake wajasiriamali kwa kuwapa fursa zilizopo ndani ya uwezo wao kwani wanawake hao huzalisha bidhaa za asili ya kitanzania ambazo hutumika ndani na nje ya nchi, na kwa kufanya hivyo huchangia kuongeza fursa za ajira na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Wito huo umetolewa …
Mama Pinda atoa zawadi ya Idd kwa yatima Dodoma
MKE wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ametoa zawadi ya Idd kwa vituo viwili vya Rahman Orphanage Centre na Kituo cha Huduma ya Neema na Uponyaji vinavyolea watoto yatima mkoani Dodoma. Zawadi hizo zenye thamani ya sh. milioni 1.4, zilikabidhiwa jana kwa niaba yake na Mwangalizi wa Makazi ya Waziri Mkuu, Bw. Dickson Nnko. Akipokea msaada huo, Katibu wa Rahman …
‘Acheni kusambaza Ukimwi’
Na Mwandishi Wetu, Makete WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambao wanajijua wameambukizwa Ukimwi wameshauriwa kuacha kusambaza ugonjwa huo kwa wengine. Sambamba na mwito huo, wamehimizwa kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari mara kwa mara ili kujitambua na kuchukua uamuzi. Ushauri huo umetolewa mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Imelda Ishuza wakati akifungua …
‘Ushauri wa Dk. Shein umeongeza ufanisi kwa watendaji’
Na Rajab Mkasaba, Zanzibar OFISI ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imeeleza kuwa maelekezo na ushauri unaotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa watendaji kila mara, umeongeza ari ya utendaji na ufanisi wa kazi. Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi uliyasema hayo katika kikao …
Kero ya maji ‘yawatibua’ nyongo wana-Ludewa
Na Mwandishi Wetu, Ludewa WANANCHI Ludewa Mjini, mkoani Njombe wamedai hawaoni umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Mamlaka ya Maji Ludewa Mjini (LUDWSSA) kwa sababu inaonekana kushindwa kutoa huduma kwa wananchi. Wakizungumza kwa nyakati na mtandao huu, wananchi hao walisema mamlaka hiyo imeshindwa kuwapatia maji ya uhakika, huku serikali ya wilaya hiyo nayo ikisuasua kuchukua hatua kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi. …