Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb), akizungumza na Balozi wa Libya nchini, Profesa, Ahmed A. El Ash’hab baada ya balozi huyo kuitwa wizarani jana kufuatia ubalozi huo kubadilisha Bendera ya nchi bila kufuata taratibu. (Picha na Tagie Daisy Mwakawago wa Wizara ya Mambo ya Nje).
CCM yampitisha mgombea Igunga, kumnadi kwa helkopta
Na Mwandishi wetu KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana jana jijini Dar es Salaam kimemteua Dk. Dalaly Peter Kafumu kuwa Mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Igunga. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, CCM imekubaliana kufanya kampeni …
Ni foleni kila ‘sehemu’ jijini Dar es Salaam
Leo maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam yalikuwa na foleni kama yalivyokutwa na mpigapicha wa dev.kisakuzi.com. Pichani ni foleni barabara ya Morogoro eneo la Magomeni Mapipa. Hii ni foleni maene ya Mtaa wa Msimbazi Kariakoo. Pichani juu ni foleni ya magari eneo la Mnazi Mmoja. Foleni barabara ya Sekilango, Sinza. (Picha zote na Joachim Mushi)
Maandalizi ya Siku Kuu ya Idd ndani ya Jiji la Dar
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakipita katika maduka anuai eneo la Kariakoo kujipatia maitaji mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Idd, ambayo huenda ikawa leo au kesho kulingana na kuandama kwa mwezi (Picha na Joachim Mushi)
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa yaadhimisha miaka 50 ya Uhuru
Na Anna Titusi – MAELEZO VYOMBO vya ulinzi na Usalama nchini Tanzania vimefanikiwa kusimamia ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na kuwawezesha wananchi kutekeleza majukumu yao katika hali ya amani na utulivu. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi wakati wa ufunguzi wa sherehe za maadhimisho …
Kanali Gaddafi ‘bado tishio’ Libya
MKUU wa waasi nchini Libya amesema, Kanali Muammar Gaddafi bado ni tishio nchini humo na duniani kwa ujumla. Mkuu wa Baraza la mpito la taifa (NTC), Mustafa Abdul Jalil amesema majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato, na washirika wengine lazima waendelee kuwaunga mkono waasi dhidi ya ‘mtawala wa mabavu.’ Waasi wameudhibiti mji mdogo wa Nofilia wakielekea …