Per Mertesacker kujiunga na Arsenal

MLINZI wa Werder Bremen anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Per Mertesacker anakaribia kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu ya Arsenal. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26- ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ya Werder Bremen inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, pamoja ya kwamba yumo katika kikosi cha timu ya taifa hivi sasa, …

Familia ya Gaddafi yakimbilia Algeria

MKE wa Kanali Gaddafi wanawe wa kiume na binti yake Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu. Balozi wa Algeria katika …

Makazi duni Tanzania, Kenya na Uganda

LICHA ya baadhi ya ripoti na taarifa za kiuchumi kutoka nchi za Tanzania, Uganda na Kenya kuonesha kuwa uchumi wa nchi hizo umekuwa ukipanda kila uchao, bado baadhi ya familia zinaishi katika makazi duni kupindukia kiasi cha kuhatarisha maisha ya familia hizo. Nchini Uganda miongoni mwa maeneo ya makazi duni na yenye msongamano kimakazi ni eneo la Katanga ambapo wakazi …

Mzee wa miaka 60 ambaka mtoto miaka 4

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamtafuta Daudi Giliama ambaye ni mzee wa umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka minne (4). Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishina Msaidizi- ACP, Diwani Athumani amesema taarifa zinaeleza tukio hilo limetokea Kijiji cha Igutwa, wilayani Kahama. Alisema mzee …

Timu ya Algeria kutua Dar Usiku

Na Mwandishi wetu TIMU ya Taifa ya Algeria (Desert Warriors) itawasili Septemba Mosi mwaka huu saa 2.50 usiku kwa ndege maalum. Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. Wambura amesema Algeria inawasili kucheza mechi ya mchujo kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika …