KAMPUNI ya kutengeneza silaha za Kijeshi ya Uingereza ‘BAE Systems’, hatimaye imekubali kuilipa moja kwa moja Serikali ya Tanzania dola milioni 47. Fedha hizo ni malipo ya ziada yaliyotokana na mauzo ya Rada ambayo yalikuwa ni zaidi ya fedha halisi ya ununuzi wa rada hiyo. Uamuzi huo unahitimisha mvutano wa muda mrefu kuhusu ununuzi wa rada hiyo ambao ulifanyika katika …
Chuo Kikuu South Carolina Marekani kushirikiana na Chuo cha Taifa Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar CHUO Kikuu cha Taifa cha South Carolina kiliopo Marekani, kimesema kitaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuendeleza uhusiano uliopo kati yake na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Hayo yalielezwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha South Carolina cha Marekani ukiongozwa na Rais wake Dk. …
Ruzuku ya mbegu, mbolea yaanza kuzaa matunda-Kikwete
Mwandishi Maalumu, Nairobi SERA ya Serikali ya Tanzania kutoa ruzuku ya mbegu na mbolea kwa wakulima wadogo wadogo wa chakula nchini imeanza kuzaa matunda kwa maana ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa chakula na hasa mahindi nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameuambia mkutano wa kimataifa. Aidha, Rais Kikwete ameitaka Jumuia ya …
Mkapa kuanza mashambulizi Igunga leo
Na Bashir Nkoromo, Igunga MWENYEKITI mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa anaunguruma leo mjini hapa atakapohutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga mkoani Tabora. Msimamizi wa shughuli za uchaguzi za CCM, Matson Chizi alisema jana kwamba mkutano huo utafanyika kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine katikati ya mji huo mdogo wa Mpanda. …
Tanzania kuiuzia Kenya tani 10,000 za mahindi
Na Mwandishi Maalumu TANZANIA na Kenya zimekubaliana kukomesha biashara ya miaka mingi ya magendo ya chakula kwenye mpaka wa nchi hiyo kwa kuamua kuuziana chakula rasmi kwa njia halali kuanzia sasa. Kwa kuanzia, Tanzania imekubali kuiuzia Kenya tani 10,000 za mahindi ili kuiwezesha nchi hiyo kukabiliana na baa la njaa linalowakabili mamilioni ya wananchi wa Kenya hasa katika eneo la …
‘FFU’ Ngoma Africa Band kuvamia Bremen City, Ujerumani
BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya “Ngoma Africa Band” aka FFU, wanatarajia kutumbuiza katika onesho kubwa la aina yake “AFRIKA MESSE” mjini Bremen, nchini Ujerumani Ijumaa ya Septemba 16, 2011 majira ya alhasiri. Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki katika kila kona duniani na mdundo wake “Bongo Dansi” made in Uswahilini. Ngoma Africa band aka FFU …