Na Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein amesema jumla ya watu 106 hadi sasa wamethibitika kupoteza maisha baada ya Meli ya abiria na mizigo ya Mv. Spice Islander usiku wa kuamkia Septemba 10, 2011. Wakati Dk. Shein akitoa taarifa hiyo, Rais wa Tanzania, Jakaya Kiwete alipowatembelea majerui jana jioni, ameelezwa …
Arsene Wenger akiri usajili ulimsumbua
ARSENE Wenger amesema alitaabika sana wakati wa msimu huu wa usajili na kuuelezea kuwa ni “usajili ulionisumbua ambao haujawahi kutokea tangu niwasili hapa”. Gunners ilimuuza Cesc Fabregas, Samir Nasri na Gael Clichy kwa klabu za Barcelona na Manchester City na wameuanza msimu huu vibaya sana, wakadhalilishwa kwa kubugizwa mabao 8-2 na Manchester United. Meneja huyo wa Arsenal amesema: “Katika kazi …
JK atuma rambirambi vifo vya wananchi katika ajali ya meli Zanzibar
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kuomboleza msiba mkubwa wa vifo vya mamia ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 10, 2011 …
Ajali ya meli Zanzibar: 163 wahofiwa kufa
WATU wasiopungua 163 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imejaa watu na mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Unguja. Inadhaniwa kuwa zaidi ya watu 500 walikuwa ndani ya chombo hicho. Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar. Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati …