Zanzibar MIILI ya watu saba waliokufa kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islanders imepatikana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mombasa huko Kenya. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd alithibitisha taarifa za kupatikana kwa miili hiyo jana wakati akipokea rambirambi kutoka kwa taasisi mbalimbali ofisini kwake Vuga, mjini hapa. …
Wakiri kuishambulia Uganda kwa mabomu
WANAUME wawili ambao walishtakiwa kwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala mwaka uliopita wamekiri makosa hayo. Wawili hao ni miongoni mwa washukiwa 14 ambao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji ya watu 70 katika mashambulio hayo. Washukiwa wa mashambulizi hayo walikuwa 19 lakini watano wakaachiliwa huru jana na Mahakama Kuu mjini Kampala. Wengine miongoni mwao raia wawili wa Tanzania …
Hatma ya madiwani waliofukuzwa Chadema kujulikana!
Na Janeth Mushi, Arusha HATMA ya Madiwani watano waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendelea na uanachama wao au la itajulikana Septemba 20 mwaka huu. Hatma hiyo itajulikana Septemba 20 baada ya mawakili upande wa wadaiwa, Method Kimomogolo na wakili upande wa wadai Severine Lawena kuwasilisha pingamizi zao mahakamani hapo kwanjia ya maandishi. Hawa Mguruta anayesikiliza kesi …
CCM yawasili Zanzibar kutoa pole ya msiba
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar UONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, umefika Ikulu mjini Zanzibar leo na kumpa mkono wa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hivi karibuni. Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa viongozi hao Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania …
TFF kuwasilisha mashtaka dhidi ya Sendeu
SEKRETARIETI ya TFF itawasilisha mashtaka dhidi ya Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi inayoongozwa na Kamishna wa Polisi mstaafu Alfred Tibaigana kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Alex Mahagi. Mara baada ya mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa …
TIKETI MECHI ZA SIMBA, YANGA CHAMAZI
TIKETI kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zinazohusisha timu za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam hazitauzwa uwanjani. Lengo ni kuwaondolea usumbufu mashabiki ambao wanakwenda kwenye mechi hizo na kukuta tiketi zimekwisha, hivyo kuweza kuwa chanzo cha vurugu. Ili kujiridhisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifanya uhakiki na kubaini …