AJALI ya ndege nchini Angola imesababisha vifo vya watu 26, wakiwemo majenerali wa kijeshi watatu, Ofisa wa Serikali ameiambia BBC. Luis Caetano, Msemaji wa Mamlaka ya Jimbo la Huambo, amesema ndege hiyo ya kijeshi ilianguka baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Huambo. Amesema watu sita wameokoka kwenye ajali hiyo, akiwemo rubani na msaidizi wake. Waandishi wa habari wamesema …
Basi lapinduka lauwa 10 na kujeruhi 19
BASI la abiria aina ya Scania lenye namba za usajili T 591 ABK (Brazila) limepata ajali leo eneo la Mwida, Ubena kilomita kadhaa ukitokea Morogoro ambapo watu 10 wamepoteza maisha. Akizungumzia ajali hiyo kutoka eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Sarehe Mbaga amesema kati ya watu waliokufa wanawake ni 7 na wanaume watatu (3). …
KCB yatoa msaada wa vifaa vya hospitali
Na Mwandishi Wetu, Mwanza BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya tiba kwa hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, iliyopo Butimba ya jijini Mwanza ili kusaidia akinamama wanaojifungua. Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4,9/- vilikabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo na Meneja wa tawi la Mwanza, Walter Lema na kupokekelewa na Mganga Mkuu Mfawidhi wa …
Kikwete ateua wakuu wa mikoa, ma-DC 11 wapandishwa kuwa RC
Na Mwandishi wetu RAIS Jakaya Kiwete amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya. Katika uteuzi huo amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa ambayo mtandao huu umeipata leo …
Bei maalumu kwa Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
Ndugu mteja wa TBC; MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA Tunaposherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika , kila mtanzania kwa namna moja au nyingine angependa kusheherekea kwa kuonyesha ni wapi tumetoka, tulipo na ni wapi tunaelekea. Taasisi za Serikali, Wizara, Mashirika na Makampuni zina fursa ya kusherehekea Sikukuu hii kwa kujitangaza na kuonyesha shughuli zao pamoja na …