Na Bashir Nkoromo, Singida KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kukamia CCM. Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA …
Picha za Uzinduzi wa Kunywa Pombe Kistarabu na SBL
KWA kile kumjali mteja na Mtanzania kwa ujumla kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni za kutoa elimu kwa raia wanaotumia vinywaji (bia aina mbalimbali zinazozalishwa na SBL), ili wanywe kistarabu bila athari yoyote. SBL inaamini wapo baadhi ya wateja wake na raia wengine ambao wamekuwa wakijisahau katika matumizi ya pombe jambo ambalo limekuwa likiwagharimu wao, familia zao na …
SBL yazindua kampeni ya unywaji wa pombe kistarabu
*Kutoa elimu nchi nzima kuwalinda raia Na Joachim Mushi WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kwa kuzindua kampeni ya kupinga unywaji wa pombe kupindukia wa pombe ambao umekuwa na madhara mengi kwa muhusika na Taifa kwa ujumla. Nahodha ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akizindua rasmi kuanza kwa kampeni hizo …
CCM waendelea kuchanja mbuga Igunga
Katibu wa Taifa wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Nchemba, akihutubia wananchi wa kijiji cha Siimbo jimboni Igunga katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo
Cameron na Sakorzy waitembelea Libya
Wazirii Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais Sakaorzy wa Ufaransa tayari wamewasili nchini Libya kufanya ziara yao. Viongozi hao wawili ndio wa kwanza kutoka nchi za magharibi, kufika Libya tangu Kanali Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani. Nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa shirika la kujihami la Nato ziliongoza operesheni za Nato kukabiliana na vikosi vya Kanali Gaddafi. Wakuu hao …
Watawala wa Libya waomba silaha kujihami!
MKUU wa Baraza la Kitaifa la Mpito nchini Libya, Mustafa Abdul Jalil ameomba vikosi vyake vipewe silaha ili waongeze juhudi zao za kuteka maeneoe mengine ya nchi ambayo yamedhibitiwa na wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi. Mustafa Abdul Jalil ameambia BBC kwamba kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani yuko kusini mwa Libya na anapanga kufanya mashambulio. Ujumbe uliondikwa na unasemekana umetoka kwa Gaddafi umeomba …