Ibrahim Masawe mchezaji bora Agosti

KIUNGO wa Timu ya Polisi Dodoma, Ibrahim Masawe amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu ya Vodacom. Masawe alichaguliwa kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo kati ya timu yake ya Polisi Dodoma na African Lyon iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu, Masawe alipata alama 93 …

Ujue Msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania inaendelea nchini. Je, wataka kujua timu gani inaongoza na nani anafunga mkia katika msimamo wa ligi hiyo? Basi BOFYA hapa chini ujue msimamo;- MSIMAMO LIGI KUU 2011-12 media

CUF wampa pole Rais Dk. Shein ajali ya meli

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar UONGOZI wa Chama Cha Wananchi, CUF umetoa mkono wa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kutoa shukurani kwa juhudi za uokozi zilizochukuliwa na serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein kutokana na kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islander hivi karibuni. Uongozi wa Chama cha …

TFF, FIFA waandaa semina kwa wadau wa soka

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) wameandaa semina ya siku tatu itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 25-28, 2011 kwenye hoteli ya Peacock. Semina hiyo inalenga kuwaleta pamoja wadau wote muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake. Wadau wakuu ni Serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wadhamini na wanahabari. Lengo …

Tanzania yafanikiwa udhibiti kemikali

Na Janeth Mushi, Arusha TANZANIA imefanikiwa kudhibiti kemikali zinaharibu hewa ya tabaka la Ozoni kwa kupiga marufuku kemikali hizo kwenye majokofu, viyoyozi vya magari na baadhi ya vipodozi. Taarifa hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Raymond Mushi, alipokuwa akifungua mkutano wa wadau anuai wa masuala ya mazingira nchini. Mkuu huyo wa wilaya alisema Tanzania imeweza …

Ongezeko la ajali barabarani zamkera Waziri

*Abuni njia mpya kudhibiti ajali Na Joachim Mushi ONGEZEKO la ajali za barabarani zimemkera Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha na sasa amependekeza utaratibu mpya ambao unaweza kudhibiti matukio mengi ya ajali hizo. Waziri Nahodha ambaye ndiye mwenye mamlaka ya usimamizi wa sheria barabarani kupitia Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, amepende sasa kuanza utaratibu …