*Atilia shaka takwimu za vocha za pembejeo Na Mwandishi Maalumu WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameonesha wasiwasi juu ya takwimu za matumizi ya vocha za pembejeo mkoani Mara hatua iliyomfanya atoe agizo la kuwepo kwa daftari la mkulima kwani ndilo litawawezesha kupata takwimu zenye usahihi. Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu Pinda jana, Septemba 16, 2011 wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa …
Pinda awacharukia wakuu wa mikoa, wilaya
*Asema wasiojua pato la wanaowaongoza hawafai Na Mwandishi Maalumu WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa wakuu wa mikoa, wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wasiojua kipato halisi cha wananchi wao hawafai kuwa viongozi katika maeneo waliyopo. Amesema kuwa kiongozi mzuri ni lazima afahamu viashiria mbalimbali kama hali za wananchi na maendeleo yao ili atambue namna ya kuwasaidia zaidi kujikwamua na hali …
Waliolipua mabomu Uganda wahukumiwa
RAIA wawili wa nchini Uganda wamehukumiwa kifungo gerezani kwa kuhusika na mashambulizi ya bomu mwaka 2010 ambayo yalisababisha vifo vya watu 76 katika mji mkuu wa Uganda Kampala. Edris Nsubuga, ambaye amekiri kutega mabomu amehukumiwa miaka 25 gerezani, ihali Muhamoud Mugisha amehukumiwa kifo cha miaka mitano kwa kuhusika katika njama ya kufanya mashambulizi hayo. Wanamgambo wa Kiislamu wa Somalia al-Shabab …
Stars, Morocco kucheza Oktoba 9
MECHI ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu nchini Morocco. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo pia ziko kundi D zitacheza tarehe hiyo hiyo na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. …