Na Mwandishi Wetu, Musoma SERIKALI imesema tayari imemtafuta Mwalimu James Irenge (120) ambaye alimfundisha Baba wa Taifa, Julius Nyerere kipindi anasoma na imeahidi kumsaidia mzee huyo matatizo mbalimbali yanayomkabili. Kauli hiyo imetolewa Septemba 17, 2011 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mabweni yanayotumiwa na watoto wenye ulemavu wa ngozi na ulemavu wa macho ya Shule ya Msingi Mwisenge iliyoko …
Wabunge Chadema Mahakamani kesho
BAADA ya juzi Jeshi la Polisi kuwahoji na kuwaachulia huru wabunge wa Chadema, jana asubuhi walikamatwa na kutupwa korokoroni hadi kesho watapokafikishwa mahakamani kujubu tuhuma za kumfanyia vurugu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.Wabunge wawili wa Chadema watakaofikishwa mahakamani kesho ni Sylivester Kasulumbai wa Maswa Mashariki na Susan Kiwanga (Viti-Maalum) pamoja na mkada wa chama hicho, Anuary Kashaga. waliwekwa …
Arsenal yalambwa 4-3 na Blackburn
BLACKBURN imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu na kumpunguzia ugonjwa wa moyo meneja wao, Steve Kean baada ya kuwa nyuma lakini wakafanikiwa kuilaza Arsenal mabao 4-3 katika uwanja wa Ewood Park. Gunners walikuwa ndio wa kwanza kupata bao lililofungwa na Gervinho kutoka umbali wa yadi 12 lakini Blackburn walisawazisha kwa bao rahisi lililowekwa wavuni …
Tume kuchunguza ajali ya meli yaundwa Zanzibar
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeunda tume maalumu huru ambayo itakuwa na jukumu la kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islanders iliyopoteza maisha ya mamia ya abiria hivi karibuni. Taarifa ya kuundwa kwa tume hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya …
Huu si wakati wa kulaumiana kufuatia ajali ya meli-Dk Shein
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema huu sio wakati wa kulaumiana wala kushtumiana kutokana na msiba mkubwa uliolipata Taifa kwa kupoteza mamia ya Wananchi kufuatia kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islandars. Badala yake wananchi wanatakiwa kuwa na subira na mshikamano juu ya mtihani huo, huku Serikali …