Mauaji makubwa yafanyika Burundi

TAKRIBANI watu 36 wameuawa baada ya watu wenye silaha wasiojulikana kufyatua risasi kwenye baa iliyojaa watu karibu na Mji Mkuu wa Burundi, Bujumbura, kwa mujibu wa maofisa wa Polisi Burundi. Wamesema idadi ya waliofariki dunia inaweza kuongezeka kwani watu wengi wamejeruhiwa vibaya kwenye uvamizi huo eneo la Gatumba. Kundi la mwisho la waasi la Burundi lilisalimisha silaha zao rasmi mwaka …

World Vision watumia bil 3.6 kuboresha shughuli za kijamii Manyara

Na Janeth Mushi, Simanjiro SHIRIKA la Misaada na Maendeleo ya Jamii ya World Vision Tanzania limetumia zaidi ya bilioni 3.6 kuboresha shughuli za kilimo, ufugaji na ujasiriamali kwa wakazi wa tarafa ya Moipo Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita. Taarifa hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora wa shirika hilo, Griffin …

Askari apigwa risasi na majambazi Arumeru

Na Janeth Mushi, Arumeru ASKARI wa Jeshi la Polisi namba F 6004, PC Prosper amejeruhiwa vibaya na risasi mapajani na majambazi wakati walipokuwa wanajibizana kwa risasi na majambazi hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha, Leonard Paul amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 2 usiku eneo la Denish Wilaya ya Arumeru barabara ya vumbi iendayo Arumeru River Lodge. Alisema …

‘Majambazi’ watatu wauwawa, wakutwa na bunduki, risasi 25

Na Janeth Mushi, Arusha WATU watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuwawa na Polisi mkoani Arusha walipokuwa wakirushiana risasi na askari hao na tayari mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusishwa na tukio hilo. Akizungumza na wanahabari jana Septemba 18, 2011 mjini hapa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Leonard Paul alisema tukio hilo lilitokea Septemba 17 mwaka huu usiku …

Vodacom yaongoza kwa wingi wa wateja, yafikisha mil 10

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Simu za mkononi ‘Vodacom Tanzania’ imefikisha idadi ya wateja milioni 10, hivyo kuwa ni kampuni pekee ya simu yenye wateja wengi nchini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hivi karibuni inaonesha Vodacom inawateja milioni 10 ikifuatiwa na Kampuni ya Airtel yenye wateja 5,927,417. Kampuni inayoshika nafasi ya tatu ni Tigo …

Pinda ataka vyombo vya dola kukagua maghala ya Sukari

Na Mwandishi Maalumu WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amevitaka vyombo vya dola mkoani Mara kufanya ukaguzi katika maghala ya wasambazaji wa sukari ili sukari hiyo ichukuliwe na kuuzwa katika maduka ya reja reja ambayo nayo yatauza kwa bei iliyoelekezwa na Serikali. Waziri Mkuu aliwataka kusimamia suala hilo kwa umakini kwa kuwa wasambazaji hao wamekuwa ni walafi wanaojali maslahi yao zaidi bila …