Wafugaji 33,422 wanufaika na mradi World Vision

Na Janeth Mushi, Arusha WAKAZI 33,422 wa jamii ya wafugaji wanaokabiliwa na tatizo la njaa wilayani Longido mkoani hapa wamenufaika na mradi toka Shirika lisilo la kiserikali la World Vision wa kutoa huduma ya msaada wa chakula kwa wananchi wanaokabilwia na tatizo hilo. SHIRIKA la World Vision Tanzania limezindua mradi wa kutoa huduma ya msaada wa chakula cha lishe kwa …

T-MOTO MODERN TAARAB YATUA DAR KUFYATUA SITA MPYA

KUNDI jipya la muziki wa taarab la Tanzania Moto Modern Taarab (T-Moto) limetua jijini Dar es Salaam leo asubuhi kutoka mfichoni katika Visiwa vya Zanzibar, lililokuwa limejichimbia kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wake uliosogezwa mbele hadi Oktoba 28 mwaka huu. Kundi hilo limewasili jijini baada ya kusitisha mazozi yake kwa muda kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa Meli …

Maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa shuleni

MAANDALIZI ya maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa Shuleni, ambayo hufanyika Septemba 28 kila mwaka duniani yamepamba moto mkoani Arusha ambapo maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kitaifa mjini hapa. Kanda ya Kaskazini ambao ni wenyeji wa maadhimisho hayo ya kitaifa,yatahudhuriwa na wadau wa uzalishaji maziwa viwandani wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo pamoja na viongozi wa kitaifa. Mwenyekiti wa …

Uzinduzi wa Vodacom Mwanza Cycle challenge

Meneja udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mbio za baiskeli “Vodacom Mwanza Cycle challenge” uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga mbio hizo zitafanyika Oktoba 22 mwaka huu zikianzia shinyanga mpaka Mwanza,katikati Mwenyekiti wa chama cha baiskeli cha Mkoa wa Shinyanga (Kamwashi) Elisha Eliasi, anaefuata ni katibu …

Dk. Bilal akizindua Kitabu cha ‘Quantum Mechanics’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi Kitabu cha ‘Quantum Mechanics’ kilichotungwa na Professa. John Kondoro, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Septemba 22, katika Ukumbi wa Chuo cha DIT, jijini Dar es Salaam. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Dodoso za sensa ya watu na makazi 2011

Mkufunzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Neema Ngure akitoa ufafanuzi wa fomu za dodoso zitakazotumika kwenye sensa ya majaribio ya watu na makazi 2011 kwa wafanyakazi watakaosimamia zoezi hilo litakalofanyika mwezi ujao katika maeneo mbalimbali nchini wakati wa semina ya mafunzo leo mjini Morogoro.