Na Janeth Mushi, Arusha KESI inayowakabili baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho taifa Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa ya kufanya kusanyiko pasipo kibali imekwama tena kuanza kusikilizwa kutokana na watuhumiwa wawili kutokuwepo mahakamani hapo Aidha kesi hiyo ambayo imekwama kuanza kusikilizwa kwa zaidi ya …
T-Moto kuwang’alisha mashabiki kwa pamba, waingia studio kukamilisha kitu!
KUNDI jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) linalotarajia kuzinduliwa Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, limezindua mavazi yake rasmi kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wake siku ya uzinduzi. Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto Blogspot, Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa wameamua kuandaa Tisheti kwa ajili ya wanaume na Vitop vya Kidada, zenye Nembo ya …
TFF wataka ufafanuzi juu ya mbwa wa polisi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko tukio la mbwa wa polisi kukata kamba na kusababisha mtafaruku kwa wachezaji wakati wa mechi kati ya Toto Africans na Simba iliyochezwa Septemba 21 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba. Tunafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ili kujua chanzo cha tukio hilo, na hatua ambazo jeshi hilo …
Madaktari 21 wa China wajitambulisha Ikulu Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Zanzibar MADAKTARI wapya 21 kutoka China wamefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kueleza kuwa watahakikisha wanatoa huduma bora kwa jamii ya Kizanzibari kwa lengo la kuinua sekta ya afya nchini. Madaktari hao wakiwa pamoja na Balozi Mdogo wa China Bi. …
Asali ya Tanzania inaubora wa kimataifa
WIZARA ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa asali ya Tanzania ni nzuri kwa matumizi ya binadamu na kuwa ina viwango vya ubora vya kimataifa. Ukweli huu umedhihirishwa na maabara mbalimbali duniani, hasa zile za Jumuiya ya Ulaya ambao ndio wanunuzi wakubwa wa asali ya Tanzania. Ufafanuzi huu unatolewa kufuatia taarifa ya hivi karibuni kupitia baadhi ya vyombo vya habari …