Nairobi MWANAHARAKATI maarufu na mtunukiwa wa tuzo ya Amani ya Nobel, Profesa Wangari Maathai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71. Mwanaharakati huyo mashuhuri wa mazingira na haki za binadamu wa Kenya Prof. Imeelezwa kuwa Wangari Maathai amefariki dunia mjini Nairobi usiku wa kuamkia, Jumatatu kutokana na maradhi ya saratani. Prof. Karanja Njoroge ambaye ni Mkurugenzi wa Green Belt …
Wanawake Saudia waruhusu kupiga kura
WANAWAKE wa Saudi Arabia hivi sasa wanabaguliwa sana, pamoja na kukatazwa kuendesha gari. Mfalme Abdullah bin Abdelaziz alisema wanawake sasa wataweza kupiga kura na piya kugombea viti, na aliongeza kusema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kushauriana na viongozi wa kidini. Mfalme wa Saudia Arabia piya alisema kuwa wanawake watakuwa na haki ya kujiunga na Baraza la Shura..baraza la mashauriano …
Dk. Shein afanya uteuzi mpya wa viongozi
Na Rajab Mkasaba, Ikulu- Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi katika nyadhifa mbalimbali, ambapo amemteua Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti wa Zanzibar. Dk. Shein pia, amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Wengine ni Bwana …
SHOOTING YAPIGWA FAINI SH. 500,000
KAMATI ya Mashindano ya TFF imeipiga faini ya sh. 500,000 timu ya Ruvu Shooting ya Mkoa wa Pwani baada ya kupata kadi sita kwenye mechi namba 40 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Septemba 17 mwaka huu Uwanja wa Mlandizi. Akitoa taarifa hiyo jana mjini hapa, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kwa mujibu wa …
MECHI YA TAIFA STARS NA MOROCCO YAHAMISHWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limehamisha mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco kutoka Casablanca na sasa itachezwa Marrakech. Mechi hiyo itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo …