Mechi ya Simba, Mtibwa zaingiza mil. 74

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa Septemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 74,345,000. Akizungumza na wanahabari leo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura amesema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 13,285 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, …

Dk. Shein aendelea kuwafariji wafiwa

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo amefanya ziara ya kuwafariji wafiwa katika Mikoa mitatu ya Unguja kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Spice Islander na kueleza kuwa serikali ina mpango wa kuijengea uwezo Idara ya Maafa ili kukabiliana na matukio na majanga mbali mbali hapa …

Pingamizi la kesi ya Lema latupwa

Na Mwandishi Wetu, Arusha MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, imetupilia mbali pingamizi zilizotolewa na wakili wa Serikali, Timon Vitalisa na Method Kimomogolo anayemtetea mdaiwa ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ya kutaka kufutwa kwa kesi ya kupinga uchaguzi wa mbunge huyo kutokana na kesi iliyofunguliwa dhidi ya Mbunge huyo na wananchi watatu na wakazi wa Arusha Mjini. …

Watakiwa kuacha mapenzi masomoni

Na Anna Nkinda – Maelezo WANAFUNZI nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kujiingiza katika mapenzi wakiwa masomoni kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao kwa kupata maambukizi ya Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Ukimwi na ujauzito. Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Kikwete wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson iliyopo Luguruni …

Kaburi la pamoja lagundulika Libya

KABURI la pamoja la mamia ya watu lagunduliwa mjini Tripoli, Libya. Kaburi la pamoja linaloaminika kuwa na miili 1,270 limegunduliwa katika mji mkuu wa Libya, Tripoli baraza la mpito la nchi hiyo limesema. Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouwawa na maafisa wa usalama mwaka wa 1996 katika gereza la Abu Salim. Uasi dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi ulianza kama …

Wenger: Kuvurunda kumeiathiri Arsenal kiuchumi

ARSENE Wenger amekiri kiwango cha chini cha soka kwa timu yake ya Arsenal kilichangia kupungua kwa mashabiki wake uwanjani wakati timu hiyo ilipocheza na Bolton siku ya Jumamosi. Lakini meneja huyo wa Arsenal ameonya kwamba mdororo wa uchumi unaoelekea kuikumba dunia huenda ukasababisha pia mashabiki kupungua katika viwanja mbalimbali vya soka England. “Kwanza tulikuwa na matokeo mabaya hivi karibuni na …