IGUNGA, KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, helikopta inayotumiwa na CCM katika kampeni za Igunga imeripotiwa kupotea ikiwa angani wakati ikijaribu kutafuta vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Dk Dalaly Kafumu. Taarifa za kupotea kwa helikopta hiyo zilianza kuzagaa jana majira ya saa tano asubuhi mjini Igunga na baadaye zilithibitishwa na mmoja wa maofisa wa CCM …
Nato yafanya mashambulizi mjini Sirte
NDEGE za kivita za NATO zimeshambulia mji wa Sirte, moja ya maeneo ya mwisho yaliyo ngome za Gaddafi, wakati wanajeshi wa serikali ya Libya wakiendelea kuushambulia mji huo. Wanajeshi wa Baraza la Mpito la Taifa la Libya (NTC) wanakabiliwa na upinzani mkali na wamepeleka vifaru kukabiliana na mashambulio ya kuvizia yanayoendeshwa na wapiganaji watiifu kwa Gaddafi. Wanajeshi wa NTC wanadhibiti …
Mtihani wa mawakala wa wachezaji wafanyika
MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) umefanyika jana Septemba 29 mwaka huu saa 4 asubuhi kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa wa Habari wa TFF, Boniface Wambura, imesema Watanzania wanane walijisajili kwa ajili ya kufanya mtihani huo. Watano …
Vodacom Foundation yatoa madawati ya mil. 45 shuleni Temeke
*Ni awamu ya pili kampeni ya madawati 1000 *Lengo kupunguza uhaba wa madawati s/msingi IKIENDELEZA utamaduni wake wa kusaidia jamii kwa lengo la kubadili maisha mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom jana ulikabidhi madawati 250 ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni ya utoaji wa madawati katika shule za msingi katika mkoa …