KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameeleza kufurahishwa na kuridhishwa kwake na amani, utulivu na uvumilivu wa kidini ulioko baina ya dini mbalimbali nchini na baina ya Watanzania wenye imani mbalimbali za kidini katika Tanzania. Pamoja na kutaka kujua hasa nini siri ya mafanikio ya utulivu na uvumilivu huo wa kidini katika Tanzania, Baba Mtakatifu pia …
Akatwa mapanga na kuchomwa moto Arusha
Na Janeth Mushi, Arusha MFANYABIASHARA wa mjini hapa amefariki dunia baada ya kupigwa, kukatwakatwa vibaya sehemu anuai za mwili na kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa kile kudaiwa kupora pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’. Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Lomayan Kisioki (37) mkazi wa eneo la Kwa Pole, lililopo Kata ya Nduruama wilayani Arumeru mkoani hapa. Tukio …
Azam FC wawalalamikia waamuzi VPL
TIMU ya Soka ya Azam FC imelalamikia vitendo vya baadhi ya waamuzi wa Soka ndani ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, kwa kile kutoa upendeleo kwa baadhi ya timu. Kwa mujibu wa taarifa na mkanda wa video ambao Azam FC imeutoa kwenye mtandao wake, imeoneshwa kutoridhishwa na mwenendo wa waamuzi kwani wamekuwa wakikandamiza baadhi ya vilabu. “Inawezekana Ngasa alikuwa offside …
Matukio mitaani
Tunapiga stori na mtasha! Mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam (aliye kaa chini) akizungumza na wageni kutoka nje ya nchi (watalii) ndani ya bustani ya eneo la Azania Front katikati ya Jiji kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Madiwani waliotimuliwa Chadema waanza vituko; Wavamia mkutano
Na Mwandishi Wetu, Arusha KATIKA hali ya kushangaza madiwani watatu waliotimuliwa uanachama ndani ya Chama Cha Maendeleo na Maendeleo (CHADEMA), na kuvuliwa nafasi zao za udiwani leo wamevamia mkutano bila ya kualikwa na kutaka kuhudhuria mkutano huo. Madiwani hao John Bayo, Rehema Mohamed (Viti maalumu) na Estomii Mallah wamefanya tukio hilo katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Polisi mjini Arusha (Police …